Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako akifungua Mkutano wa Nne wa mwaka
wa Mtandao Jamii mjini Dodoma jana (Jumatano, 30/10/2019). Mkutano huo
wa siku sita ulioanza Jumatatu wiki hii (28/10/2019) umeandaliwa Jumuiya
ya Mtandao wa Intaneti, the internet society (ISOC) kwa kushirikiana na
Association for Progressive Communication (APC) na Chuo Kikuu cha
Dodoma.
Washiriki wa kongamano la Jumuiya
ya Mtandao wakifuatilia ufunguzi rasmi wa Mkutano wa Nne wa mwaka wa
Mtandao Jamii mjini Dodoma jana (Jumatano, 30/10/2019). Mkutano huo wa
siku sita ulioanza Jumatatu wiki hii (28/10/2019) umeandaliwa Jumuiya ya
Mtandao wa Intaneti kwa kushirikiana na Association for Progressive
Communication (APC) na Chuo Kikuu cha Dodoma.
……………………..
Serikali ya Tanzania inatambua
umuhimu wa kuwekeza katika mawasiliano kama mkakati
mmojawapo wa
kuhakikisha azma ya kuwa nchi ya uchumi wa kati kupitia viwanda
inafikiwa
Hayo yameelezwa na Waziri wa
Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako alipomwakilisha
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa
katika ufunguzi wa Kongamano la Nne la Huduma ya Mtandao Jamii
linalofanyika katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ambapo amesema sekta
ya mawasiliano ni moja ya sekta zinazochangia kwa kiasi kikubwa katika
ukuaji wa uchumi nchini.
“Kwa kipindi cha Julai hadi
Desemba 2017 sekta ya mawasiliano ilikua kwa asilimia 13.1 na ilikuwa
sehemu ya pili katika kuchangia ukuaji wa uchumi nchini,” amesema
Profesa Ndalichako.
Profesa Ndalichako amesema katika
kuhakikisha huduma za mawasiliano zinafika mpaka vijijini, mwaka 2014
serikali iliingia mkataba na kampuni kutoka Vietnam wa kuhakikisha
huduma hiyo inafika katika vijiji 4,000 ambapo kufikia Januari 2019,
vijiji vyote vilikuwa vimefikiwa na huduma hiyo.
Waziri huyo ameendelea kuelezea
kuwa serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) imefanya
kazi kubwa katika kuhakikisha inafikisha mawasiliano vijijini ambapo
mpaka sasa imeweza kupeleka huduma ya mawasiliano katika Kata 562 zenye
vijiji 2,132.
Aidha, Profesa Ndalichako amesema
kwa upande wa elimu, mfuko huo umewezesha kufika kwa huduma za
mawasiliano katika baadhi ya shule na taasisi za kielimu pamoja na kutoa
mafunzo ya huduma za mawasiliano kwa walimu wapato 1,229.
Akizungumza katika Kongamano hilo
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Profesa Faustine Bee
amesema kongamano hilo linatoa nafasi kwa washiriki kujifunza namna ya
kuendelea kuboresha huduma ya mawasiliano kwa jamii hasa jamii ambayo
haijafikiwa na huduma hiyo.
“Lengo kubwa ni kuhakikisha
ifikapo 2025 taasisi zote za serikali ziwe zimefikiwa na huduma ya
mawasiliano ikiwemo vyuo vyote, shule zote za msi ngi na sekondari
pamoja na ofisi zote za serikali,” amesema Profesa Bee.
Kongamano hilo la wiki moja
linahusisha nchi za Afrika ambazo ni wanachama wa Internet Societ
Association for Progressive Community na ufanyika mara moja kwa mwaka,
ambapo kwa mwaka huu limefanyika nchini Tanzania likiwa na washiriki
kutoka Kenya, Uganda, Liberia, Cameroon, Ghana, Spain na mwenyeji
Tanzania.
No comments :
Post a Comment