
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akikata utepe kuzindua mwongozo wa
Wataalam wa Maendeleo ya Jamii nchini mara baada ya kufungua Kongamano
la Mkutano Mkuu wa mwaka wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii kushoto kwake ni
Rais wa wa CODEPATA Bw. Sunday Wambura na kulia kwake ni Bw. Patrick
Golwike Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara yake.

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akitoa hotuba yake kwa Kongamano
la Mkutano Mkuu wa mwaka wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii.

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akikata utepe kuzindua chama cha
wataalam wa maendeleo ya jamii nchini CODEPATA mara baada ya kufungua
Kongamano la Mkutano Mkuu wa mwaka wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii.

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akipokea zawadi iliyotolewa kwake
na chama cha Wataalam wa Maendeleo ya Jamii nchini CODEPATA mara baada
ya kufungua Kongamano la Mkutano Mkuu wa mwaka wa Sekta ya Maendeleo ya
Jamii.

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akikagua banda la Wizara yake mara
baada ya kufungua Kongamano la Mkutano Mkuu wa mwaka wa Sekta ya
Maendeleo ya Jamii.

Baadhi ya Wataalam wa Sekta ya
Maendeleo ya Jamii wakifuatailia jambo kwa umakini wakati wa Kongamano
la Mkutano Mkuu wa mwaka wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW
……………..
Na Mwandishi Wetu Dodoma
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amewataka wataalam wa Maendeleo ya
Jamii nchini kujiongeza katika utendaji kazi wao na
kuhakikisha
wanakuwa na takwimu sahihi za matukio ya ukatili badala ya kutegemea
taarifa za Jeshi la Polisi ambazo utolewa na Mkuu wa Jeshi hilo baada ya
mwaka mzima.
Waziri Ummy amesema hayo leo
Jijini Dodoma wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Wataalam wa maendeleo
ya Jamii linaloendelea kwa siku mbili kama sehemu ya Mkutano Mkuu wa
mwaka wa wataalam wa maendeleo ya jamii.
Waziri Ummy amesema wataalam
wenzao wa afya wamekuwa wakimpatia taarifa zenye takwimu kwa wakati na
kuwataka wataalam hao kuiga mfano huo kwa kuwataka kuwa wanawasiliana na
vituo vya polisi mkoani kwao ili waweze kupata taarifa za waanga wa
ukatili katika maeneo yao kazi.
“Kila nikienda katika ziara sipewi
taarifa yoyote kutoka kwa wataalam wa maendeleo ya jamii na hata
nikiwauliza unakuta hawana taarifa yoyote ile kuhusina na masuala
yanayohusiana na masuala ya Maendeleo ya Jamii.’’ Aliongeza Waziri Ummy.
Kufuatia hali hiyo Waziri Ummy
amemwagiza Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Nchini Bw. Patrick
Golwike kuweka mfumo mzuri wa kukusanya takwimu za maendeleo ya jamii
ili kuwezesha kupatikana kwa takwimu izo kwa muda na kwa haraka.
‘’Nikija katika Mkoa au
Halmashauri yako nipate takwimu, ukiongea na takwimu ni rahisi kupata
rasilimali fedha na misaada mingine itakayosaidia kutatua changamoto
zilizopo mfano kupata takwimu za vikundi vya wajasiliamali ambao
wamepokea mikopo ya Halmashauri’’. Aliongeza Waziri Ummy.
Pamoja na kutoa changamoto hizo
kwa wataalam hao Waziri Ummy amewataka wataalam hao kuhamasisha jamii
ili iweze kutumia teknolojia ya habari kwa ajili ya kujiletea maendeleo
na kuongeza kuwa kwa kutumia taarifa zinazopatikana jamii itapata
taarifa za masoko ya bidhaa zao ikiwemo namna bora ya kulima kwa
utaalam.
Aidha Waziri Ummy ameitaka jamii
kuacha kutumia muda mwingi kufuatilia mitandao ya kijamii na badala yake
wahamasishwe kutumia muda wao mwingi kwa mambo yenye tija ikiwemo ari
ya kuchangia jamii kwa ajili ya maendeleo.
Waziri Ummy ameitaka jamii ya
watanzania kuwa inapenda starehe sana na watu wanatumia fedha nyingi
kwa ajili ya kusherekea harusi, siku ya kuzaliwa bila kujiuliza kama
fedha hizo zinaendana vipaumbele ambavyo mtu amejiwekea au kuchangia ada
kwa ajili ya mwanafunzi.
Waziri ummy ameitaka jamii kutumia
teknolojia hiyo kufanya mambo yenye tija na akitoa mfano wa wataalam wa
maendeleo ya jamii kuendelea kuhamasisha jamii kuwekeza katika elimu ya
Afya ili tuweze kupata huduma bora katika jamii.
Aidha amewataka wataalam hao
kufikilia kuwekeza sana katika miradi ambayo ina mashiko na kukemea
tabia ya wafadhili kuweka mkazo katika masuala ya warsha na Semina
ambazo hazitoi matokeo ya moja kwa moja katika jamii.
Akizungumza kwa Niaba ya katibu
Mkuu Maendeleo ya jamii, Mkurugenzi wa maendeleo ya Jamii bw.Patrick
Golwike amseme ajukuu kubwa la wataalam wa Maendeleo ya Jamii ni
kuiandaa jamii ushiriki katika shughuli za maendeelo ya nchi.
Kwa upande wake Rais wa Chama cha
Wataalam wa Maendeleo ya Jamii Bw. Sunday Wambura amesmea kuwa Mkutano
Mkuu wa mwaka huu umekuja na uzinduzi wa Chama chao kitakachowasaidia
kupeana mbinu mbalimblia za kuhakikisha maafisa wanaisaidia jamii katika
kujiletea maendeleo.
Wataalamu wa Sekta ya Maendeleo ya
Jamii wanakutana Jijini Dodoma katika Mkutano Mkuu wao wa mwaka kwa
lengo la kukumbushana majukumu yao lakini pia kupata maarifa mapya
kutoka mada mbalimbali zitakazotolewa katika mkutano huo wa siku nne.
No comments :
Post a Comment