
Afisa Viwango Mwandamizi
Bw.Mathias Missanga akitoa elimu kwa wadau waliotembelea banda la TBS
katika maonesho ya Viwanda, Biashara na uwekezaji linaloendelea katika
Mkoa wa Pwani.
TBS imetumia fursa hii kutoa elimu ya Viwango kwa wajasiriamali na wananchi kwa ujumla.
TBS imetumia fursa hii kutoa elimu ya Viwango kwa wajasiriamali na wananchi kwa ujumla.
********************************
Na Mwandishi Wetu, Pwani
WAFANYABIASHARA na wajasiriamali
mkoani Pwani wametakiwa kujitokeza kwa
wingi kwenye ofisi za Shirika la
Viwango Tanzania (TBS) kwa ajili ya kuthibitisha ubora wa bidhaa
wanazozalisha ili kuondokana na vikwazo vya kibiashara ndani na nje ya
nchi.
Ushauri huo ulitolewa jana Ofisa
Uhusiano wa TBS, Neema Mtemvu, wakati akizungumza washiriki wa Wiki ya
Viwanda, Uwekezaji na Biashara mkoani Pwani iliyoanza Oktoba 17, mwaka
huu ikitarajiwa kufikia kilele chake kesho (Oktoba 23).
Mtemvu, alisema shirika hilo
limeshiriki wiki hiyo Viwanda, Uwekezaji na Biashara kwa ajili ya kutoa
elimu ya viwango kwa wafanyabiashara na wajasiriamali hasa kuhusiana na
umuhimu wa kupata alama ya ubora.
Alisema kwa wajasiriamali gharama za kupata alama za ubora ni bure, kwani tayari zinalipwa na Serikali.
Alifafanua kwamba kinachotakiwa ni
wajasiriamali kupata barua ya utambulisho kutoka Shirika la Kuhudumia
Viwanda Vidogo (SIDO) na kuipeleka TBS, ambapo mchakato wa kuwapatia
alama ya ubora unaanza mara moja.
Mtemvu, alisema shirika hilo inatambua mchango wa
wajasiriamali katika kukuza pato la taifa na kutengeneza ajira kwa
wananchi wengi, ndiyo maana kuna mchakato endelevu wa kutoa elimu kwa
wajasiriamali kwa kuwa na hilo ni sehemu ya majukumu ya shirika ili
waweze kupata alama ya ubora.
Alisema katika kuelekea uchumi wa
viwanda ni lazima kuzingatia viwango, ndiyo maana wamekuwa wakishiriki
maonesho mbalimbali ikiwemo wiki ya Viwanda, Uwekezaji na Biashara
mkoani Pwani
kwa ajili ya kutoa elimu.
kwa ajili ya kutoa elimu.
Mtemvu alitoa wito kwa
wajasiriamali akisema suala la wao kukidhi matakwa ya viwango vya
kitaifa kwa bidhaa wanazozalisha na zinazosindikwa ni la msingi kwa kuwa
ndiyo njia pekee ya kupanua wigo wa masoko ya bidhaa zao ndani na nje
ya nchi.
“Kwa hiyo uwepo wetu hapa ni fursa
muhimu ambayo inamlenga kumwinua mzalishaji aweza kushindana na kuuza
bidhaa zake bila woga,” alisema Mtemvu.
Alitoa mwito kwa wananchi wa Pwani na nchini kote kwa ujumla kuhakikisha wanatumia bidhaa zenye ubora.
Wakati huo huo, Mtemvu alisema
wiki hiyo ya Viwanda, Uwekezaji na Biashara wameitumia kama fursa kuwapa
taarifa washiriki kuwa baadhi ya majukumu yaliyokuwa yakitekelezwa na
iliyokuwa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) ya chakula na
vipodozi sasa hivi yamehamia TBS.
“Serikali ya Awamu ya Tano
imeliona hilo na kwa hatua hiyo sasa inakuwa ni rahisi mno kupata alama
ya ubora, kwani ukishapata alama ya ubora utaweza kufanya biashara na
vile vile ule mzunguko uliokuwepo awali wa kuzunguka wa kwenda TFDA
halafu urudi TBS utakuwa umepungua,” alisema Mtemvu
No comments :
Post a Comment