
Japhet Birunda Mkurugenzi Mkazi
wa kampuni ya Addscoin Tanzaniaakizungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake Mikocheni jijini Dar es salaam wakati alipoelezea uzinduzi
wa Sarafu ya Kidigitali utakaofanyika Oktoba 26,2019.

Bw. Richard Charles Mhandisi na
mtaalamu wa Block Chain na Capital Currency akizungumza namna Sarafu
hiyo ya kidigitali inavyoweza kufanya kazi.

Japhet Birunda Mkurugenzi Mkazi
wa kampuni ya Addscoin Tanzania na Fred Mushi Katibu Mtendaji wa Kamuni
ya Addscoin Tanzania Ltd na maafisa wengine wakiwa kwenye mkutano huo.
…………………………………………..
Kamuni ya Addscoin Tanzania Ltd
imeanzisha mradi wa kutoa huduma ya elimu juu ya
technologia mpya ya
Block Chain unaosarisha fedha kwa njia ya Mtandao katika kuendeleza
uchumi wa viwanda ambapo pia inanahamasisha watu kuwekeza kwenye mradi
wa IRA (Insetive Research Africa) ambao malipo yake yanatumia sarafu
Diligence ya kidigitali .
Hayo yamesemwa na Japhet Birunda
Mkurugenzi Mkazi wa kampuni ya Addscoin Tanzania wakati akizungumza na
waandishi wa habari katika ofisi za kampuni hiyo zilizopo Mikocheni
jijini Dar es salaam.
Amesema kampuni ya Addscoin
Tanzania Ltd imeunda mfumo wa kusaidia kutunza sarafu za Kidigitali
Bitcoin , Ethelium, na Diligence ambayo itatumiwa na watanzania
wanaotumia msaada wa Block Chain kusafirisha na kutunza fedha. pia mfumo
huu utasaidia serikali kujua kiwango cha pesa zinazotunzwa na
watanzania kwenye Sarafu Digit.
Bw. Japhet ameongeza kuwa Kampuni
hiyo iko katika mazungumza na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kama
msimamizi mkuu wa taasisi za kifedha ili kuona namna itakavyoweza
kufanya kazi na kutekeleza majukumu yake hapa nchini.
Ameongeza kuwa Oktoba 26 .2019
kwenye hoteli ya Akemi jijini Dar es salaam kampuni hiyo pia itazinduwa
kampeni ya mfuko wa utunzaji mazingira duniani “Green Care for Future
Life” utakaochangiwa na mataifa yote duniani kwa msaada wa Block Chain
Technolog na sarafu Digit sambamba na uzinduzi wa Exchanger Platform
Wallet iitwayo “Sell Bitcoin
Japhet amesema kwa kushirikiana
na taasisi ya kijamii inayoratibu mazingira Tanzania (WETAAIFICO
watahamasisha jamii kushiriki katika utunzaji wa mazingira duniani pote
kwa msaada wa (Block chain).
Uzinduzi huo utaambatana na
mkutano mkubwa utakaojumuisha wadau wote wa maendeleo ya kiuchumi kutoka
sekta zote nchini ili kutambua fursa kwa wawekezaji na kutambua
tekinologia mpya ya kuwekeza na kupata faida maradufu ya kidijitali.
Kwa heshima na taadhima
tunawaalika kufanya mawasiliano ili kupewa utatibu mzuri zaidi wa namna
ya kuhudhuria mkutano huo bila kukosa. tayari nafasi zimechukuliwa na
zilizobaki ni chache tu.
Kampuni Addscoin Tanzania Ltd
isajiliwa kisheria kwa usajiri Namba 139341325 kutangaza na kuuza pamoja
na kuendesha (Block Chain Technolog na sarafu Digital) ina vibali vya
kuendesha biashara hiyo kisheria kutoka Brela ili kubuni miradi ya
kibiashara kwa msaada wa Block Chain inayoweka mazingira kwa washiriki
wote kulipa kodi.
No comments :
Post a Comment