
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu, Sera, Bunge, Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista
Mhagama (katikati) akimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS)Bi. Roida Andusamile
wakati alipotembelea Banda la Shirika hilo siku ya kilele cha maonesho
ya Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) yaliyofanyika
mkoani Simiyu Oktoba 14- 20 2019.Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Baraza
hilo Bi Beng’i Issa.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS)Bi. Roida Andusamile
akisisitiza jambo kwa baadhi ya wanafunzi na wananchi waliotembelea
Banda la Shirika hilo wakati wa kilele cha maonesho ya Baraza la Taifa
la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) yaliyofanyika mkoani Simiyu
Oktoba 14- 20 2019.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS)Bi. Roida Andusamile
akigawa vipeperushi kwa sehemu ya wananchi waliotembelea Banda la
Shirika hilo wakati wa kilele cha maonesho ya Baraza la Taifa la
Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi yaliyofanyika mkoani Simiyu Oktoba 14- 20
2019.
(Picha zote na TBS)
…………………….
Na Mwandishi Wetu- TBS
Shirika la Viwango Tanzania (TBS)
limetakiwa kushirikiana na Shirika la Kuhudumia
Viwanda Vidogo (SIDO)
kuwawezesha wajasiriamali kupata maeneo bora ya kuzalishia katika
karakana za SIDO.
Waziri wa Nchi , Ofisi ya Waziri
mkuu, Sera, Bunge, Kazi,Vijana, Ajira na Walemavu, Mhe. Jenista Mhagama
ametoa wito huo jana mkoani Simiyu alopotembelea banda la TBS wakati wa
kilele cha maonesho ya tatu ya mifuko ya uwezeshaji program na vikundi
vya kifedha yaliyoandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi
kiuchumi.
Mhe.Mhagama alitoa wito huo
kufuatia maelezo kutoka kwa afisa wa TBS Bi. Roida Andusamile kuwa
wajasiriamali wengi wanashindwa kuthibitisha ubora wa bidhaa
wanazozizalisha kutokana na kutokuwa na majengo bora ya kuzalishia.
“TBS mnapaswa kushirikiana na
SIDO ili kuwawezesha wajjasiriamali kuzalishia katika kalakana za SIDO
na hatimaye waweze kuzalisha kwa kuzingatia viwango na kuthibitisha
ubora wa bidhaa hizo”,alisisitiza Mhe. Mhagama.
Akizungumza na washiriki wa
maonesho hayo Mhe. Mhagama ameitaka mifuko inayotoa mikopo kwa
wajasiriamali kuongeza kasi ya utoaji wa mikopo hiyo ili iweze kufikia
wajasiriamali wengi nchini.
Mhe. Mhagama alisema utoaji huo
wa mikopo uwe na riba nafuu ili wajasiriamali wengi wanufaike nayo na
amelitaka Baraza la Uwezeshaji kusimamia mifuko ya uwezeshaji kuendelea
kujitambulisha na kujitangaza kwa wananchi kupitia programu mbalimbali.
Naye mtenndaji Mkuu wa Baraza
hilo Bi. Beng’I Issa amewataka wananchi wa Simiyu kuchangamkia fursa
zinazotokana na maonesho hayo kwani uwepo wa maonesho hayo utaibua
chachu ya maendeleo kwa wananchi wa Simiyu.
Alisema maonesho haya pia
yanakutanisha wajasiriamali na taasisi za serikali lengo likiwa ni
kuwawezesha kurasimisha biashara zao na kuhamasisha matumizi ya mifuko
ya ya kijamii pamoja na mtandao kwa wajasiriamali.
Maonesho haya yaliyoanza Oktoba
14,2019 mpaka Oktoba 20 2019 mbali na wajasiriamali yameshirikisha
taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi zipatazo 48
Katika maonesho hayo TBS ilipata
fursa ya kuwatembelea wajasiriamali wapatao 60 wanaozalisha bidhaa
mbalimbali na kuwapatia utaratibu ili waweze kusajili majengo
wanayozalishia , bidhaa na kuthibitisha ubora wake.
Pia wananchi waliotembelea banda
la TBS walielimishwa umuhimu kwa kutumia bidhaa zilizothibitishwa ubora
na TBS na kuangalia muda wa matumizi wa bidhaa wanazozinunua badala ya
kuangalia bei.
No comments :
Post a Comment