
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo
ya Jamii wa Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick
Golwike (kulia) pamoja na Afisa Tarafa ya Dodoma Bi. Neema
Nyalege wakishirikiana na baadhi ya wataalam wa Maendeleo ya Jamii na
wananchi wa Kata ya Iyumbu kushiriki ujenzi wa Maabara ya Shule ya
Sekondari Iyumbu Mkoani Dodoma.

Afisa Tarafa ya Dodoma Bi. Neema
Nyalege akikabidhi kiasi cha shilingi Milioni moja kama harambee ya hapo
hapo kwa Afisa Mtendaji wa Kata ya Iyumbu kuchangia ujenzi wa maabara
ya Shule ya Sekondari Iyumbu Mkoani Dodoma wakati wa zoezi la kuamsha
ari ya wananchi kujiletea maendeleo iliyoendeshwa shuleni hapo na
wataalam wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii Nchini.

Baadhi ya wataalam wa Sekta ya
Maendeleo ya Jamii Nchini wakishiriki zoezi la kuamsha ari ya wananchi
kujiletea maendeleo iliyofanyika shule ya Sekondari ya Iyumbu leo Jijini
Dodoma.

Baadhi ya wataalamu wa Sekta ya
Maendeleo ya Jamii Nchini wakishiriki zoezi la kuamsha ari ya wananchi
kujiletea maendeleo iliyofanyika shule ya Sekondari ya Iyumbu leo Jijini
Dodoma.

Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya
Jamii Dkt. Bakari George akishiriki zoezi la kuamsha ari ya wananchi
kujiletea maendeleo iliyofanyika shule ya Sekondari ya Iyumbu leo Jijini
Dodoma na Wataalam wa Maendeleo ya Jamii.

Baadhi ya wataalam wa Sekta ya
Maendeleo ya Jamii Nchini wakishiriki zoezi la kuamsha ari ya wananchi
kujiletea maendeleo iliyofanyika shule ya Sekondari ya Iyumbu leo Jijini
Dodoma.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW
…………………
Na Mwandishi Wetu Dodoma
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo
ya Jamii wa Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick
Golwike amesema kimsingi jukumu la wataalam wa Maendelaeo Nchini sio
tu
kutoa mikopo kwa vikundi vya uwezeshaji wananchi kiuchumi bali ni
kuchechemua ari ya wananchi kujiletea maendeleo kwa kutumia rasilimali
walizonazo.
Bw. Golwike amesema hayo
Mkoani Dodoma katika Kata ya Iyumbu wakati wa zoezi la wataalam wa Sekta
ya Maendeleo ya Jamii kushiriki ujenzi wa maabara ya Shule ya Sekondari
Iyumbu iliyoko nje kidogo ya Jiji la Dodoma ikiwa ni mwendelezo wa Wiki
ya Mkutano Mkuu wa wataalam wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii.
Bw. Golwike ameviambia vyombo
vya habari kuwa ushiriki wa zoezi la ujenzi wa vyumba vitatu vya maabara
ya shule hiyo endeshwa na wataalam wa sekta ya maendeleo ya jamii ni
utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Jamii ya mwaka 1996 kwa
vitendo kwani sera hiyo inawataka wananchi kujiletea maendeleo kwa
kutumia rasilimali zilizopo.
Naye Afisa Tarafa ya Dodoma
Bi. Neema ambaye alisoma hotuba yake kwa wataalam hao kumwakilisha Mkuu
wa Wilaya ya Dodoma Bw. Patrobas Katambi amesema pamoja na jitihada za
Serikali kuhamasisha jamii kujiletea maendeleo bado mwamko wa jamii
kutumia rasilimali zilizopo kujiletea maendeleo bado huko chini.
Bi. Neema aliongeza kuwa kwa wataalam hao kutambua mwitikio
huo mdogo kwa jamii ndio maana wameamua kushirikiana na wananchi wa kata
ya Iyumbu kujenga maabari hiyo ya vyumba vitatu ili kuamsha ari ya
wananchi kushiriki kujiletea maendeleo.
Bi. Neema aliitaja hatua hiyo
kuwa ya kupongeza kwani imetekeleza kwa vitendo Sera ya Taifa ya
Maendeleo ya Jamii ya mwaka 1996 inayohimiza wananchi kujiletea
Maendeleo kwa kutumia rasilimali zilizopo.
Aidha Bi. Neema amewataka wanafunzi shuleni hapo kusoma
masomo ya Sayansi ndio maana wataalam hawa wako hapa ili kuchangia
ujenzi wa maabara yao kwa lengo la kuwapa hamasa wanafunzi shuleni hapo
kusoma sayansi kwa vitendo badala ya nadharia ili hapo baadae waweze
kulisaidia taifa katika fani ya sayansi na teknolojia.Aidha Bi. Neema amepongeza jitihada zilizofanywa na uongozi wa chama cha taaluma ya Maendeleo ya Jamii maarufu CODEPATA kwa kujitolea ujenzi wa vyumba vya maabara lakini pia kutoa mifuko ya saruji 120 kwa ajili ya ujenzi wa maabara hiyo itakayogharimu kiasi cha takribani milion 200 mpaka kukamilika kwake.
Mtendaji wa kata ya Iyumbu Bw.
Vicent Leo ameitaja Kata yake kuwa moja ya Kata 41 zinazounda Jiji la
Dodoma yenye wakazi elfu 6.5 hivyo kuongeza kuwa ujenzi wa Sekondari
Iyumbu haukwepeki ili kupunguza hadha ya wanafunzi kwenda mwende mrefu
kufuata elimu mbali na Kata yake.
Bw. Leo amezitaja gharama za
ujenzi wa Maabara hiyo kuwa ni gharama ya takriban milioni 200 mpaka
sasa kiasi cha fedha ambacho kimetumika ni shilingi milioni 32 ikiwemo
michango ya wananchi pamoja na fedha kutoka ofisi za kata hiyo .
Wakati huo huo Rais wa Chama
cha Wataalam wa fani ya Maendeleo ya Jamii Nchini Bw. Sunday Wambura
wakati akiongea na wananchi wa kata ya Iyumbu pamoja na wataalam wenzake
amesema kazi ya wataalam wa maendeleo ya jamii ni kukaa na kula na
wananchi na baadae kufanya kazi pamoja nao kufanya kazi lengo la
kujiletea maendeleo.
‘’Dhana kubwa ya maendeleo ya jamii ni kuamsha hari ya
wananchi kujiletea maendeleo na unaweza kuona kama hatujafanya kitu sana
lakini tumeokoa shilingi milioni sita ambazo wananchi wa kata hii
wangelazimika kuzitumia ili kutekeleza kazi hii’’Aliongeza Bw. Wambura.
Naye Mkazi wa kata ya Ijumbu Bi.
Janeth David amewashukuru wataalam wa Maendeleo ya Jamii kwa kuja
kuwaunga mkono juhudi zaoza kujenga shule na maabara ili kuwakomboa
watoto kutembea umbali wa kilometa 24 kufuata huduma ya elimu katika
Shule ya Sekondari Kisasa.
Wataalamu wa Sekta ya
Maendeleo ya Jamii wanakutana Jijini Dodoma katika Mkutano Mkuu wao wa
mwaka kwa lengo la kukumbushana majukumu yao lakini pia kupata maaraifa
mapya kutoka mada mbalimbali zitakazotolewa katika mkutano huo wa siku
nne.
No comments :
Post a Comment