Naibu Waziri wa Uchukuzi na
Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (aliyetangulia mbele) akitoka
kukagua mnara (unaoonekana pichani nyuma) wa kijiji cha Mlaga, kata ya
Nyampande wakati wa ziara yake ya kukagua upatikanaji wa huduma za
mawasiliano, Sengerema mkoani Mwanza
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John
Mongella akiwa ofisini kwake akifurahi baada ya kukabidhiwa na Naibu
Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (kushoto)
kitabu chenye orodha ya minara iliyojengwa na UCSAF. Kulia ni Waziri wa
Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa
Naibu Waziri wa Uchukuzi na
Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye akisisitiza jambo kwa viongozi
wa Mkoa wa Mwanza wakati wa ziara yake ya kukagua upatikanaji wa huduma
za mawasiliano mkoani humo. Wa kwanza kulia ni Waziri wa Viwanda na
Biashara, Innocent Bashungwa na katikati ni Mkuu wa Mkoa huo, John
Mongella
Wananchi wa Nyampande
wakimsikiliza Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi
Atashasta Nditiye (hayupo pichani) akiwahamasisha kusajili laini za simu
zao kwa alama za vidole wakati wa ziara yake Sengerema, Mwanza
Naibu Waziri wa Uchukuzi na
Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye akihamisha wananchi wa Nyampande
kusajili laini za simu zao kwa alama za vidole wakati wa ziara yake
Sengerema, mkoani Mwanza
…………………………..
Na Prisca Ulomi, Mwanza
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania imetenga shilingi bilioni 65 kwa ajili ya kujenga minara ya
mawasiliano kwenye maeneo mbali mbali nchini ili kuongeza upatikanaji wa
huduma za mawasiliano kwa lengo la kukuza uchumi na kufanikisha utoaji
wa huduma za
Serikali kwa wananchi, wananchi waweze kuwasiliana wenyewe
kwa wenyewe, kuwasiliana na Serikali yao na kurahisisha uendeshaji wa
shughui za kijamii
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa
Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye wakati akikagua
upatikanaji wa huduma za mawasiliano kwenye kata ya Nyampande iliyopo
wilayani Sengerema mkoani Mwanza.
Mwenyekiti wa kijiji cha Malaga
kilichopo kwenye kata ya Nyampande, Mathayo Thobias ameishukuru Serikali
kwa huduma ya mawasiliano wanayoipata kwa kuwa wameingia kwenye
mawasiliano bila kusua kusua baada ya kusimikwa kwa mnara wa mawasiliano
kwenye kata hiyo na amekiri kuwa mnara wanafurahia uwepo wa mnara huo
kwa kuwa mbali na kuwapatia huduma za mawasiliano pia umekuwa chanzo cha
mapato ya kijiji ambapo Serikali ya kijiji inapata shilingi milioni 3.6
ambazo inalipwa na kampuni ya Vodacom inayomiliki mnara huo
Nditiye amesema kuwa, tayari
Serikali imetenga jumla ya shilingi bilioni 65 za kujenga minara ya
mawasiliano ipatayo 1,222 kwenye kata 521 sehemu mbali mbali nchini
nzima kwa kuupa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) ruzuku ya kuzipa
kampuni za simu za mkononi fedha hizo kupitia utaribu uliowekwa, kwa
kuzingatia vigezo na masharti ya zabuni ambapo UCSAF ilitangaza zabuni
ya kujenga minara hiyo na kampuni za simu ziliomba zabuni hizo ili
kujenga minara hiyo nah ii karibuni watapatiwa fedha hizo ili kuanza
ujenzi wa minara
Akiwa ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa
Mwanza, John Mongella, alipofika kumsalimu, Nditiye alisema kuwa lengo
la Serikali ni kuhakiisha kuwa Sekta ya Mawasiliano inaongeza mchango
wake kwenye pato la taifa kwa kuongeza kiwango cha uchangiaji kutoka
asilimia 13.1 kwa mwaka 2017/2018 kwa kushika nafasi ya tatu
“Hapa tulipo wote tuna simu za
mkononi na hakuna atakayekaa zaidi ya nusu saa bila kushika simu yake ya
mkononi,” amesema Nditiye. Amefafanua kuwa lengo la Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano ni kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa ya mfano na
tayari nchi nyingi za Afrika zinajifunza kwetu kwa Sekta ya Mawasiliano
na dhamira ya Serikali ni kuendeleza Sekta hii ili kwenda sambamba na
nchi zilizoendelea duniani ambapo hadi sasa Tanzania iko vizuri kati ya
nchi chache za Afrika kama vile Afrika Kusini na Mauritius kwa upande wa
mawasiliano
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John
Mongella amemweleza Nditiye kuwa mkoani kwake usikivu wa mawasiliano uko
vizuri, mawasiliano yanasikika kwa kiwango cha juu sana ukilinganisha
na kipindi cha nyuma
“Zamani hata likitokea tukio
inachukua wiki kufahamu ila sasa ni saa chache tu tunapata taarifa na
kushughulikia,” amesema Mongella. Nikiri wazi kuwa mawasiliano
yamesogeza wananchi karibu na Serikali yao
Akiwa ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa
Mwanza, Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa amemweleza
Nditiye kuwa Sekta ya Mawasiliano ni Sekta wezeshi, sisi Sekta yetu ya
viwanda na biashara inategemea sekta yako ya mawasiliano na inatuwezesha
kuingia na kutumia fursa ya soko la pamoja la jumuiya ya Afrika
Mashariki na SADC, hivyo kuongeza soko la ajira na kukuza uchumi wa
taifa letu na kwa vile Mwanza ni mkoa wa kimkakati ni dhahiri kuwa
mawasiliano yanaongeza chachu ya biashara
Naye Mkuu wa Kitengo cha Uchaguzi
wilayani Sengerema, Ashura Kajuna alimueleza Nditiye maara alipowasili
ofisini kwa Mkuu wa Wilaya hiyo kuwa kumekuwa na shida ya upatikanaji wa
vocha za mtandao wa TTCL hivyo amemuomba Nditiye kuhakikisha kuwa vocha
hizo zinapatikana kwa kuwa huduma za za sauti na data TTCL ni za
gharama nafuu ukilinganisha na kampuni nyingine
Nditiye amesema kuwa ni jukumu la
taasisi za Serikali kupeleka mahitaji kwa wananchi kuendana na matakwa
yao, hivyo ameliagiza Shirika la TTCL kuhakikisha kuwa kila palipo na
laini za simu za TTCL kuwe na vocha.
Naye Katibu Tawala wa Wilaya ya
Sengerema, Allan Augustino, amemuomba Nditiye kuhakikisha kuwa maeneo ya
pembezoni yanapata huduma za data ili kuweza kufanikisha huduma za
intaneti adala ya kupata huduma za sauti tu
Nditiye anaendelea na ziara yake
mkoani humo ya kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano, kuhamasisha
wanachi wasajili laini za simu zao na kutekeleza mpango wa anwani za
makazi na postikodi
No comments :
Post a Comment