
*****************************
NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
MKOA wa Pwani
umewathibitishia wawekezaji wanaowekeza kwenye mkoa huo kuwa mitaji yao
italindwa kwani nchi ina amani na ni sehemu salama kwao.
Hayo yalibainishwa
,mjini Kibaha na Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo
alipokuwa akizungumza na viongozi wawili wa serikali na wajumbe watatu
chemba ya biashara kutoka Jimbo la Hebei nchini China walipotembelea
maonyesho ya biashara za viwanda yanayofanyika wilayani Kibaha
Alisema kuwa ugeni
huo ulikuja kwenye maonyesho hayo kwa ajili ya kuangalia kama wataweza
kuwekeza na aliwahakikihia kuwa Tanzania ni nchi nzuri na ina usalama wa
kutosha na mitaji yao itakuwa salama hivyo wasiwe na hofu juu ya
usalama wa mitaji yao.
Ndikilo
alieleza,wageni hao toka Hebei nchini China waliakwa kupitia kampuni ya
Cpl inayomilikiwa kwa pmoja na raia wa China na raia wa Tanzania
inayojihusisha na usagaji wa mahindi ili kupata unga kiwanda ambacho
kiko wilayani Kibaha mkoani humo.
“Tumewahakikishia
kuwa nchi yetu iko vizuri usalama wa kutosha na mitaji yao itakuwa
salama kwani hata walipotembelea kwenye benki za NMB na CRDB
wamethibitishiwa usalama wa mitaji yao endapo watakuja kuwekeza,”
alisema Ndikilo.
“Jimbo la Hebei
limeendelea kwenye viwanda vikiwemo vile vya vya simenti kwani walianza
kuzalisha mnamo mwaka 1889 na linaongoza duniani kwa kuzalisha chuma
ambapo moja ya tisa cha chuma duniani kinazalishwa kutoka jimbo hilo,”
alisema Ndikilo
Wamewekeza kwenye
nchi 90 duniani na Afrika wamewekeza kwenye nchi 27 na imewekeza miradi
127 nchi za kwenye nchi za Afrika kabla ya kuondoka wataangalia kwenye
mwongozo wa uwekezaji wa mkoa .
“Hadi sasa jimbo la
Hebei wamewekeza kwenye viwanda vitatu kwenye mkoa wa Pwani wamepita
kwenye mabenki na kituo cha uwekezaji cha TIC na EPZA na wamefurahishwa
sana na fursa zilizopo,” alisema Ndikilo.
No comments :
Post a Comment