Wafanyakazi wa Benki ya NMB Kanda
ya kati wakiangalia mashuka na wafanyakazi wa Hospitali ya Wilaya ya
Kiteto Mkoani Manyara muda mfupi baada ya benki hiyo kukabidhi msaada wa
vifaa tiba wenye thamani ya zaidi ya milioni tano hospitalini hapo.
Baadhi ya Wananfunzi wa Shule ya
Sekondari ya Chief Sarwat ya Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara wakibeba
viti na meza muda mfupi mara baada ya kukabidhiwa msaada huo na Benki ya
NMB wenye thamani ya shilingi milioni tano shuleni hapo.
…………………………
Benki ya NMB imetoa msaada wa
madawati 215 katika shule za sekondari Mahenge, Vigoi na
Isongo zilizoko
Wilayani Ulanga mkoa wa Morogoro na Ng’hoboko iliyoko Wilayani Meatu
Mkoani Simiyu.
Mbali na hilo benki hiyo pia
imetoa msaada wa vifaa tiba katika hospitali ya Wilaya ya Kiteto vyenya
thamani ya shilingi milioni tano ambapo vifaa hivyo vilivyotolewa ni
pamoja na vitanda na mashuka na magodoro.
Msaada huo wa madawati umegharimu
kiasi cha sh. Milioni 20, ambapo katika shule za Wlaya ya ulanga benki
hiyo imetoa madawati 165 yaliyogharimu Milioni 15 huku katika shule ya
Ng’hoboko imetoa madawati 50 ambayo yamegharimu Milioni 5.
Vifaa hivyo pamoja na madawati
vimetolewa kwa nyakati tofauti ndani ya wiki hii, ambapo vinaifanya
benki hiyo kuchangia katika shughuli za maendeleo jumla ya shilingi
Milioni 675 hadi sasa kwa mwaka huu tu.
Meneja wa benki hiyo kanda ya
Magharibi Sospeter Magesse akiongea katika hafla ya kukabidhi madawati
shule ya Ng’hoboko alisema kuwa msaada huo umetolewa ili kuwawezesha
wanafunzi wasome vizuri.
Alisemakuwa benki hiyo imekuwa
ikitenga kiasi cha sh. Bilioni moja kila mwaka kwa ajili ya kurejesha
kwa wananchi, pesa ambayo imekuwa ikitumika kuboresha huduma za elimu,
na afya.
“ NMB kama benki ya watanzania
itaendelea kusaidiana na serikali pamoja na watanzania katika kuboresha
huduma za afya na elimu, tuna imani kwa msaada huu wanafunzi watajisomea
vizuri,” alisema Magesse.
Naye Nsolo Mlozi Meneja wa benki
hiyo kanda ya kati akikabidhi vifaa tiba katika hospiali hiyo alisema
kuwa NMB inatoa msaada huo kama njia ya kurudisha faida kwa wananchi
ambao ndiyo wateja wao wakubwa.
“ Ingawa Serikali inafanya
makubwa, Benki hiyo inao wajibu wa kuunga mkono juhudi hizo za maendeleo
kwa kusaidia jamii kwani kupitia jamii hii hii, ndio imeifanya benki
NMB kuwa hapa ilipo na kubwa kuliko benki yoyote hapa nchini,” Alisema Mlozi.
“ Vifaa hivi vya tiba na afya
tunavyokabidhi leo ni moja ya ushiriki wetu katika maendeleo ya jamii na
sisi kama benki inayoongoza Tanzania tunahakikisha jamii inayotuzunguka
inafaidika kutokana na faida tunayoipata,” aliongeza Mlozi.
Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Mkoani
Morogoro Ngolo Malenya akipokea madawati ameishukuru benki ya NMB kwa
kutoa madawati 165 kwa ajili ya wanafunzi wa shule za sekondari za
mahenge ,vigoi na isongo
Ametoa wito kwa wanafunzi hao
kuwa mabalozi kwa wazazi wao kwa kuwaeleza mambo mazuri yanayofanywa
na benki hiyo ili pia wazazi hao waiunge mkono benki hiyo kwa kufungua
account mbalimbali ili NMB izidi kurudisha faida wanazopata kwa jamii
kwa kuleta maendeleo.
Naye Mkuu wa wilaya ya Meatu Dkt
Joseph Chilongani aliishukuru benki ya NMB huku akitaka wanafunzi wa
shule hiyo na walimu kuhakikisha madawati hayo yanatunzwa ili kudumu kwa
muda mrefu.
“ Kuna haja ya kuweka adhabu
kidogo kwa wale ambao watahusika kuaribu haya madawati, akiaribu
mwanafunzi yeye au mzazi wake wahusike katika kutengeneza, tunataka haya
madawati yatumiwe na wadogo zetu ili waone umuhimu wa NMB,” Alisema Chilongani.
No comments :
Post a Comment