Monday, September 2, 2019

WATAALAMU WA MANUNUZI NCHINI WATAKIWA KWENDA SAMBAMBA NA MFUMO MPYA WA MANUNUZI KUOKOA FEDHA ZA UMMA


Na Ahmed Mahmoud Arusha
Wataalamu wa sekta ya manunuzi ya umma nchini wametakiwa kwenda na mfumo mpya wa manunuzi ili k kuendana na mnyororo wa wa thamani ya fedha wenye uwazi utakaosaidi serikali kutekeleza bajeti kwa kuokoa na kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato.
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Arusha Fabian Daqarro wakati akifungua
mafunzo ya wataalamu wa sekta ya manunuzi juu ya mfumo mpya wa manunuzi ya umma kwa njia ya mtandao na kuzitaka taasisi za serikali kuchangamkia fursa ya kuleta wataalamu wao kupata mafunzo hayo.
Alisema kuwa mfumo huo utasaidia sana kuondoa misururu maofisini na kuipunguzia serikali gharama na hivyo mnyororo wa thamani ya fedha kuonekana na kuwapunguzia kutopatikana kwa nwazabuni wasioendana na miradi pia wao kuwapunguzia majukumu ya ufuatiliaji wazabuni hao wanaotekeleza miradi na huduma chini ya viwango kila uchwao.
“Najua wapo wengine watachukia ila kuweni na uzalendo kwa kuwa mfumo huu utawasaidia kuondoa dhana potofu iliyojengeka kwa upande wenu na utajenga usawa wa kuwapata wazabuni wenye ubora na sifa sahihi hali itakayopelekea kuokoa fedha za serikali”
Alitanabaisha kuwa mfumo huo ni kama moyo wa serikali hivyo mafunzo mtakayoyapata ni matarajio yangu yataenda kuleta mafanikio chanya nikiamini kuwa wapiga dili hawataupenda mfumo huu kwa kuwa matumizi mabaya ya serikali yanaanzia huko kwenye manunuzi ya umma.
Awali akimkaribisha mkuu wa wilaya Mtendaji mkuu wa mamlaka ya
usimamizi wa manunuzi ya umma PPRA mhandisi Leonard Kapongo alisema kuwa mafunzo hayo ni ya awamu ya nne tokea kuzinduliwa kwa mfumo huo ambao upo kisheria na utasaidia kuongeza uwelewa ili kutekeleza jukumu la takwa la kisheria.
Alisema kuwa jumla ya washiriki 220 kutoka taasisi 71 wanapatiwa
mafunzo hayo kwa siku sita awali mafunzo hayo yalianza kwa taasisi 80 kutoka mikoa mitano tokea mwezi wa nane mwaka huu na kusema kuwa hii ni awamu ya nne tokea mafunzo hayo kuanza na yanatolewa bure.

No comments :

Post a Comment