| Mkurugenzi wa Taasisi Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa TBL, Philip Redman Katika hafla ya kukabidhi printer 9 iliyofanyika Jijini Dar es Salaam. |
NA MWANDISHI WETU
Kampuni
ya TBL Group chini ya kampuni mama ya ABInBEV, imetoa msaada wa Printer
9, kwa taasisi ya Tulia Trust, ikiwa ni kuunga mkono jitihada
zinazofanywa na taasisi hiyo kukabiliana na changamoto mbalimbali za
kijamii hususani katika kuboresha sekta ya elimu nchini.
Hafla ya kukabidhi msaada msaada huo ilifanyika jijini Dar es Salaam na
kuhudhuriwa na Mkurugenzi wa Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson, Mkurugenzi Mkuu wa
TBL, Philip Redman ,na baadhi ya wafanyakazi kutoka taasisi hizo.
Akiongea katika hafla hiyo,Dk.Tulia, alishukuru kampuni ya TBL kwa
jitihada ambazo imekuwa ikifanya kusaidia kukabiliana na changamoto za
kijamii.
Akiongelea msaada huo, Meneja wa Masuala Endelevu wa TBL, Irene
Mutiganzi, alisema kuwa kampuni hiyo itaendelea kuunga mkono jitihada za
serikali na taasisi nyingine za maendeleo kushirikiana kupambana na
changamoto mbalimbali kwenye jamii, hususani katika sekta ya elimu kama
ambavyo inaendelea kutoa msaada wa Printer na vifaa vya kurahisisha
elimu mashuleni.
Mkurugenzi
wa taasisi Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson na Mkurugenzi Mkuu wa TBL, Philip Redman,
wakibadilishana mawazo Katika hafla hiyo
No comments :
Post a Comment