Na.Alex Sonna,Dodoma
NI UTHUBUTU ndio
umepelekea kupiga hatua moja kwenda nyingine, hayo ni maneno ya
Mjasiriamali Sella Mkisi ambaye ni Mkurugenzi wa Unique & Superior
Bakery jijini hapa inayojihusisha kutengeneza vitafunwa na kusambaza
katika maeneo ya ndani na nje ya jiji la Dodoma
Ni kama hadithi
lakini ni ukweli usiopingika kutokana na Mjasiriamali Sella Mkisi ambaye
anasema mafanikio yake yametokana na juhudi za Shirika la kuhudumia
viwanda vidogo nchini (SIDO)
ambalo limechangia
kwa kiasi kikubwa kumtoa hatua moja kwenda nyingine, katika suala zima
la ukuaji kiuchumi katika ujasiriamali anaofanya.
Alifanyaje mpaka
kufikia hapo ni baada ya kupeleka wazo lake la kutaka kujifunza
kutengeneza mikate maandazi pamoja vitu mbalimbali akitumia fursa ya
uwekezaji katika maeneo mbalimbali ambayo mkoa umeyaainisha na kutoa
fursa kama mjasiriamali unaona unaweza kumudu na kuingia kwenye
ushindani wa soko la kimataifa kadri siku zinavyokwenda kujitokeza
kuwekeza.
Wazo lake la
kutengeneza vitafunwa kama mikate,maandazi na keki lilionekana kuwa lulu
baada ya kuongeza ujuzi SIDO,na baada ya kuhitimu mafunzo yake alianza
kuchukua mkopo wa laki tano toka SIDO kama mtaji wake wa kutengeneza
mikate,maandazi na baadae keki ambazo anaziuza sehemu mbalimbali hapa
jijini na nje ya jiji la Dodoma.
Ni kama mzaha alianza lakini kadri siku zinavyokwenda anazidi kutanua wigo wa ujasiriamali anayofanya.
Katika mahojiano na
Mkurugenzi wa Unique & Superiol Bakery Sella Mkisi anasema hakuna
kitu kikubwa kama uthubutu,ukijaribu kitu unachotaka kufanya basi ni
lazima kitafanikiwa kwa sababu tayari umeweka nia ya kusudio lako ambalo
unahitaji kufanya katika ujasiriamali.
Anasema ukifanya
hivyo ni dhahiri kwamba unahitaji kupata mafanikio katika biashara
yoyote unayotaka kufanya isipokuwa uzingatie nini unahitaji kuwekeza.
Akisimulia Sella
anasema yeye alianza na mtaji wa laki tano tu lakini ndoto yake ni kuwa
Mjasiriamali mkubwa katika biashara ya mikate na maandazi anayofanya
hivi sasa hapa jijini pamoja na kusambaza nje ya jiji la Dodoma na
inaonekana kupendwa na watu wengi kwa ajili ya matumizi ya kila siku.
“Nivigumu kuamini
hiki ninachosema lakini ni ukweli nashauri vijana wenzangu kuwa na
uthubutu wa kile wanachofikiria kufanya wafanye wasisite,” amesema
Sella.
Anasema hivi sasa
taifa linaelekea katika uchumi wa kati wa viwanda hivyo ni vema vijana
wengi kuweka uthubutu katika ujasiriamali wanaofikiria kufanya ili
kutumia fursa ambazo zinatangazwa na jiji la Dodoma ili kuweza kusonga
mbele katika kile wanachofikiria kufanya badala ya kusubiri ajira toka
serikalini au kampuni yoyote binafsi.
Anasema kinachotakiwa
ni kufikiria jinsi gani ya kufanya katika ujasiriamali unaohitaji
kufanya ikiwemo kutumia fursa za mikopo ambazo zinatolewa na taasisi
mbalimbali hapa nchini ili kufikia lengo unalohitaji kufanya
No comments :
Post a Comment