Meneja wa Mauzo na Biashara wa TBL Afrika mashariki Bi.Edith Bebwa,akiongea wakatiwa mahafali hayo.
Baadhi ya wahitimu wa mafunzo hayo yaliyowalenga zaidi wamiliki wa mabaa na Mameneja wao wakipokea vyeti vya ushiriki
Wahitimu katika picha ya pamoja wakati wa mahafali hayo
………………
Kampuni ya Bia Tanzania
chini ya kampuni ya kimataifa ya ABInBEV, Mwishoni mwa wiki iliwatunuku
vyetiwahitimu waMafunzo ya kukuza Biashara kwa wajasiriamali wadogo
yaliyoendeshwa katika mikoa ya Dar es Salaan na Dodoma.
Haya ni mahafali ya pili
tangu kuanzishwa kwa programu hii ya kukuza biashara kwa wajasiriamali
wadodo hapa Tanzania mwaka Jana, 2018.
Akizungumza katika hafla
hiyo, Meneja wa Mauzo na Biashara wa TBL Afrika Mashariki Bi.Edith Bebwa
alisema, “Programu hii ambayo inajulikana zaidi kama RDP, imefanikiwa
kuwafikia washiriki 183 ikiwa ni ongezeko la 11% ukulinganisha na mwaka
jana. Wengi wa washiriki ni wamiliki na wasimamizi wa baa mbalimbali
kutoka katika mikoa hii miwili ya Dar es salaam na Dodoma.
“Leo tarehe 26 Septemba
2019, tunayo furaha kuwatunuku vyeti wajasiriamali hawa wa Dar es salaam
waliopata mafunzo kwenye wilayani zao yaani Temeke (iliyojumuisha
Temeke na Kigamboni),Kinondoni,Ubungo na Ilala.Washiriki hawa wamepatiwa
mafunzo yaliyoandaliwa na kufundishwa kitalaam ili yaweze kusaidia
kuendelezana kukuza biashara zao na hatimaye kuchangia zaidi uchumi wa
taifa kupitia kodi na ajira. Mafunzo haya yalitolewa katika namna mbili,
moja mafunzo ya nadharia darasani na pili mafunzo na ushauri katika
maeneo yao ya biashara”. Alisema Bebwa.
Kwa upande wake kiongozi
wa TAPBDS taasisi iliyosimamia uendeshaji wa mafunzo hayo Ndugu Joseph
Migunda alisema, “Mafunzo haya yana maudhui yaliyoendana na utendaji na
mahitaji katika aina hizi za biashara. Mzunguko wake umechukua takribani
miezi minne kuanzia mwezi wa Sita hadi wa Tisa. “Tunaimani kwamba wengi
wa washiriki watanufaika nayo na tayari tunashuhuda mbalimbali kwa
baadhi yao ambao wamechukua hatua tofauti na kufanyia kazi elimu na
ushauri waliopata kwa ajili ya maboresho. Tunashukuru ubunifu huu wa TBL
na uamuzi wao wa kutumia wataalamu wetu katika kuwezesha haya yote.”
Alisema
No comments :
Post a Comment