Rais Magufuli amemualika Rais
Museveni wa Uganda katika ufunguzi wa mkutano mkubwa wa Wafanyabiashara
kati ya Uganda na Tanzania ambao utawashirikisha wafanyabiashara zaidi
ya 1000 ambao watapata nafasi ya kujadili namna ya kuongeza biashara
mpya baina ya
nchi hizi Mbili.
Hayo yamesemwa na Waziri wa
Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa wakati akizungumza na waandishi
wa habari alipokuwa akihamasisha wafanyabiashara wa Tanzania kujitokeza
Kwa wingi kushiriki katika kongamano hilo linalotaraji kufanyika
Septemba 6,2019 katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Bashungwa amesema kongamano hilo
litafunguliwa na Rais Yoweri Museven wa Uganda litagudhuriwa pia na
mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe
Magufuli
Aidha Waziri Bashungwa Ametoa
wito kwa wafanyabiashara wa mikoa ya kanda ya ziwa ambao wengi wao ndio
wamekuwa wakifanya biashara Moja kwa Moja na nchi za jirani hili waweze
kupata mtandao mpya wa kibiashara.
Ametaja na kusema muungano wa
kimtandao baina ya Tanzania na Uganda utafungua njia mpya ya Biashara
hadi Sudan ya kusini ambao wamekuwa wakifanya biashara na Uganda kila
uchwao.
Amesema muungano wa kibiashara
baina ya nchi hizi Mbili utaongeza mabilioni kwa nchi yetu ya Tanzania
kwani mpaka Sasa sisi ndio tumekuwa tukiuza zaidi kwao kuliko wao kuuza
kwetu.
Amesema kuwa Uganda imekuwa
ikitegemea mazao ya chakula kutoka hivyo wauzaji wa nafaka na
Wasindikaji wa vyakula wanatakiwa kutumia fursa hii vizuri kwa kutanua
masoko yao.
No comments :
Post a Comment