Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya mafuta ya Puma Energy
imeunga mkono kampeni ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ya
kuokoa maisha maisha watoto wanaogua ugonjwa wa moyo kwa
kuchangia
Shilingi milioni 40 ili kufanikisha upasuaji kwa watoto 20.
Mbali na kutoa fedha hizo kwa
ajili ya kusaidia matibabu ya moyo kwa watoto hao, Kampuni hiyo ya
mafuta ya Puma Tanzania imetoa zawadi kwa shule ya Msingi Kibamba pamoja
na mwanafunzi wa shule hiyo kwa kushinda mchoro wa elimu ya usalama
barabarani.
Akizungumza leo Septemba 30,2019
jijini Dar es Salaam wakati wa kikabidhi fedha hizo Mkurugenzi wa Puma
Energy Dominic Dhanah, amesema hatua ya kuunga mkono kampeni hiyo ni
kuhakikisha wanaokoa maisha ya watoto ambao wazazi wao hawana uwezo wa
kugharamia matibabu.
Amesema kampuni hiyo inatambua
dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano katika kusadia makundi yenye
mahitaji maalum na ndio maana wameona kuna kila sababu ya kumuunga mkono
Makonda katika kusaidia matibabu ya watoto wenye matatizo ya moyo ambao
wanahitaji kufanyiwa operesheni.
Kuhusu mafunzo ya usalama
barabarani kwa watoto wa shule za msingi, amesema yamesaidia kupunguza
ajali katika maeneo ambayo wametoa mafunzo hivyo wanaamini kwa kufanya
hivyo wanaokoa kizazi cha sasa na kijacho kwa kuwa elimu ya matumizi
bora ya barabara inaendelea kusambaa.
Ameongeza kuwa lengo kubwa la
mpango huu ni kuwafanya watoto hao kuwa na uelewa wa matumizi ya
barabara wakiwa bado wadogo. “Tunaamini kwa kufanya hivyo tunawaongezea
uelewa kuhusu dhima nzima ya usalama barabarani kwa wa Tanzania wengi
zaidi,” amesema Dhanah.
Amesema kazi hiyo kwa mwaka huu
imefanyika katika mikoa ya Dodoma na visiwani Zanzibar ambapo jumla ya
shule 34 zitafikiwa kwa mpango huu kwa mwaka 2019.
“Lengo letu kama kampuni ni
kuongeza wigo ili kufikia shule nyingi Zaidi nchi nzima. Pia tutaendelea
kuwekeza katika kampeni ya usalama barabarani ikishirikiana na serikali
kupitia Jeshi la Polisi ili kuokoa maisha ya Watanzania,” amesema.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema kuwa Kampuni ya Puma, imetoa kiasi
cha Sh milioni 40 kwa ajili ya kugharamia matibabu ya watoto 20 ambao
wanahitaji kufanyiwa upasuaji wa moyo lakini wazazi mwao hawana uwezo wa
kulipia matibabu.
“Puma wameonesha njia ya kujali na
kutusaidia kwenye moyo. Niliomba msaada huo katika mkutano wa SADC.
Nina watoto 500 pale Muhimbili wanaumwa moyo.
“Mimi nikialikwa mahali ninaomba
msaada kwa wananchi wangu. Dominic wa Puma nilimuomba na gharama za
matibabu kwa kila mtoto ni Shilingi milioni mbili kwa kiasi hiki cha
fedha Shilingi milioni 40 sasa tunakwenda kurudisha tabasabu kwa watoto
20.
“Watapata operesheni kwakuwa
sehemu ya faraja na mafanikio kwa mtoto atakayefanyiwa opesheni. Hata
nilipokutana na Balozi wa Dubai baada ya kumueleza hili, yeye alikwenda
kuleta madaktari ambao walifanya upasuaji wa matibabu kwa watoto 50.
“Mwezi ujao nitaunda kamati ya
watu saba kwa ajili ya kusaka Shilingi bilioni moja, ili mpaka tukifika
Desemba mwaka huu watoto wote wawe wamefanyiwa upasuaji,” amesema
Makonda
Kuhusu idadi ya watu wanaopata ajali za barabarani, alisema kuwa kwa sasa imepungua kutokana na elimu ya usalama barabarani.
“Tuna imani watoto 1m atakuwa
na uelewa iwapo wataelimishwa na wenzao. Watumia vyombo vya moto
watambue kila mmoja ana jukumu la kufuata usalama barabarani. Kabla ya
Desemba kutakuwa na check up ya bure kwa wanaotaka kwenda likizo.
“Mafundi wa bure watakuwapo,
nataka waende vizuri kula likizo na warejee tena Dar wakiwa salama.
Trafiki kwenye mwendokasi inafanya vibaya,” amesisitiza.
Hata hivyo Makonda aliagiza kukamatwa kwa madereva wanaotumia barabara za mwendokasi.
“Wanatumia barabara ya
mwendokasi wakamatwe hakuna gari, pikipiki wala mtu anayepaswa kuitumia,
Mwakyoma (RTO), apeleke trafiki hapo,” ameongeza.
Kwa kukumbusha tu mpaka sasa
wanafunzi zaidi ya 20,000 shule za msingi katika shule tisa za Jiji la
Dar essalaam wamepata mafunzo ya usalama barabarani ambapo katika
mashindano hayo Shule ya Msingi Kibamba iliibuka mshindi wa kwanza na
kuzawadiwa Sh.milioni nne.
No comments :
Post a Comment