Saturday, September 28, 2019

PROFESA BENNO NDULU, GAVANA WA BENKI KUU (MSTAAFU) APEWA HESHIMA KUBWA NA RAIS WA AFRIKA KUSINI


NA K-VISA BLOG/Mashirika ya Habari
GAVANA wa zamani wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Beno Ndulu (pichani) ni miongoni mwa wanazuoni 18 walioteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Mhe. Cyril Ramaphosa kuunda Baraza la Rais la Ushauri wa Kiuchumi (Presidential Economic Advisory Council-PEAC) litakaloanza kazi kuanzia POktoba Mosi, 2019.
Katika taarifa yake msemaji wa Rais wa Afrika Kusini, Bw. Khusela Diko iliyotolewa Septemba 27, 2019 na kuchapishwa kwenye mtandao wa Ikulu ya Afrika Kusini mjini Pretoria, imesema Rais Cyril Ramaphosa ametangaza Baraza hilo wakati akilihiuyibia taifa.na wajibu mkubwa wa Baraza ni kumshauri Rais kuhusu masuala ya kiuchumi.
“Likiwa limeundwa na mchanganyiko wa wasomi kutoka ndani ya Afrika ya Kusini na nje ya nchi hii baraza litamshauri Rais na Serikali kwa mapana yake, kuwezesha maendeleo ya utengenezaji wa sera zitakazoshamirisha uchumi jumuishi” Alisema msemaji huyo wa Ikulu ya Afrika Kusini na kuongeza….Baraza hili sio la kisheria na litakuwa huru na Mwenyekiti wake ni Rais na litwajumuisha pamoja wachumi maarufu, wanazuoni, kutoka taaisisi binafsi, Kazi na Wafikirishi wa Kijamii na kwamba watafanya kazi hiyo kwa kujitolea kwa muda wao na watafidiwa ili kuweza kujikimu ikiwa ni pamoja na gharama za usafiri wakati watakapokuwa wakitekeleza majukumu hayo kwa kipindi cha miaka mitatu.

No comments :

Post a Comment