
Mahakama
ya Gauteng ya nchini Afrika Kusini imeamuru ndege ya Shirika la ndege
Tanzania (ATCL) aina ya Airbus A220-300 iachiliwe.
Akizungumza
na waandishi wa habari mahakamani hapo leo Septemba 4, 2019, Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na
Kimataifa Dkt. Damas Ndumbaro amesema leo katika video inayoonekana
mitandaoni kuwa "Mahakama imetoa maamuzi yake kwa kuiachilia ndege ya
Tanzania iliyokuwa imekamatwa hapa na kwamba hoja zote zilizoletwa na
mawakili wetu zimekubalika kwahiyo tumeshinda kesi hiyo na imeamriwa
kuwa ndege hiyo inaweza kuondoka." Alisema Dkt. Ndumbaro katika
mahojiano hayo yanayoonekana kwenye ukanda wa video.
Alisema,
mahakama imesema kama kuna hoja yoyote ile ya Bw.Hermanus Steyn anaweza
kwenda kuifungua Tanzania kwasababu alikuja huku akisema kwamba kuna
maamuzi ya msuluhishi lakini maamuzi ya msuluhishi yameshabadsilishwa na
hukumu ya mahakama kwa hiyo amri ya mahakama ya Tanzania inaweza
kutekelezwa na mahakama za Tanzania sio mahakama za Afrika Kusini.
Hata
hivyo Naibu Waziri ameshangazwa na hatua ya Bw. Steyn ya kufungua kesi
nyingine kupinga hukumu hii kabla haijasomwa na tunashangaa Bw. Steyn
alijuaje kwamba hukumu hii itatoka dhidi yake yeye mpaka anakata rufaa
tena hata kabla ya hukumu yenyewe kusomwa maana amekata rufaa jana
wakati hukumu imesomwa leo kwahiyo sisi tunashangaa, lakini tunaishukuru
mahakama ya Afrika Kusini kwa uamuzi wake na tunawashukuru Watanzania
wote ambao wameunga mkono juhudi zetu za kuianasua ndege hii.
No comments :
Post a Comment