Thursday, September 5, 2019

MKUTANO WA SIKU TANO WA KUJADILI MIKAKATI YA USALAMA WA KUHIFADHI MABAKI YA VYANZO VYA MIONZI WAENDELEA JIJINI ARUSHA

Mkuu wa kitengo cha uhifadhi wa mabaki ya vyanzo vya mionzi, katika Tume ya Nguvu za Atomic (TAEC) Nchini, Bw. Mikidadi Swalehe, akizungumza na waandishi wa habari.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa majadiliano ya namna ya kutatua changamoto na namna ya kuhifadhi  na kuboresha usalama wa mabaki ya vyanzo vya mabaki ya mionzi wakifuatilia kilichokuwa kikijadiliwa jijni Arusha.

Mwakilishi wa Shirika la Nguvu za Atomiki, Duniani, Bw. David  Bannet  David  Bannet  akitoa salamu za shirika hilo ambalo ni mwangalizi wa Kimataifa wa masuala ya matumizi ya teknolojia ya nyuklia
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa majadiliano ya namna ya kutatua changamoto na namna ya kuhifadhi  na kuboresha usalama wa mabaki ya vyanzo vya mabaki ya mionzi wakifuatilia kilichokuwa kikijadiliwa jijni Arusha.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa majadiliano ya namna ya kutatua changamoto na namna ya kuhifadhi  na kuboresha usalama wa mabaki ya vyanzo vya mabaki ya mionzi wakifuatilia kilichokuwa kikijadiliwa jijni Arusha.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa majadiliano ya namna ya kutatua changamoto na namna ya kuhifadhi  na kuboresha usalama wa mabaki ya vyanzo vya mabaki ya mionzi wakifuatilia kilichokuwa kikijadiliwa jijni Arusha.

Na Vero Ignatus,Arusha.
Mkutano wa Kimataifa  wa siku tano kujadili mikakati mbalimbali ya kuboresha usalama katika kuhifadhi mabaki ya vyanzo vya mionzi, unaendelea Jijini Arusha.

Mkutano huo  unakutanisha wataalam wa teknolojia ya nyuklia kutoka sehemu mbalimbali duniani ili kujadili changamoto za usalama wakati wa uhifadhi wa mabaki hayo, kwa nia ya kuepusha madhara kwa binadamu  na mazingira

Mkuu wa kitengo cha uhifadhi wa mabaki ya vyanzo vya mionzi, katika Tume ya Nguvu za Atomic (TAEC), Bw. Mikidadi Swalehe amesema  mkutano huo unahudhuriwa na wanachama 30, kutoka nchi 21 duniani, ambapo umelenga katika kujadili mikakati ya namna ya kudhibiti vyanzo vilivyomaliza muda wake lakini bado vinatoa mionzi.

 Bw. Mikidadi alisema jukumu la kusimamia usalama linahitaji nchi zote duniani, kuhakikisha kwamba, vyanzo vyote vya mionzi vinakuwa katika mikono salama, ili kuepuka madhara mbalimbali ikiwemo kutumika kwa vyanzo hivyo katika masuala ya ugaidi.
Alisema vyanzo vya mionzi vilivyomaliza matumizi vinahitajika kuhifadhiwa mahali salama  palipo na ulinzi maalum, kwani hali hiyo itasaidia kuepusha vyanzo hivyo kuzagaa na kusababisha madhara mbalimbali kwa binadamu na mazingira.

"Sisi kama TAEC tunalo jengo maalumu kwaajili ya kuhifadhia vifaa hivyo vilivyomaliza matumizi yake." Alibainisha Bw. Mikidadi.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani (IAEA)  Bw. David  Bannet  akitoa salamu za shirika hilo ambalo ni mwangalizi wa Kimataifa wa masuala ya matumizi ya teknolojia ya Nyuklia,a liishukuru Tanzania hususani TAEC kukubali kuwa mwenyeji wa mkutano huo.
Aidha amesisitiza kuwa  IAEA  itaendelea kushirikiana na nchi wanachama kuhakikisha kuwa teknolojia ya nyuklia inatumika kwa matumizi  salama ili isiathiri binadamu wa vizazi vilivyopo sasa na vijavyo.
Awali mkutano huo wa siku tano ulifunguliwa na Mkurugenzi mkuu wa TAEC Nhini Profesa Lazaro Busagala ambapo unatarajiwa kumalizika leo.

No comments :

Post a Comment