Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa
na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi
wa Operesheni wa Chuo cha Maendeleo na Ushirikiano wa Kimataifa (MS
TCDC) Bw. Andreas Anderson (Katikati) alipowasili katika chuo hicho kwa
ajili ya ufunguzi wa Tamasha la Kiswahili leo Jijini Arusha.
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa
na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akiingia katika ukumbi wa
Maendeleo na Ushirikiano wa Kimataifa ( MS TCDC) ufunguzi wa Tamasha la
Kiswahili leo Jijini Arusha.
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa
na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akiongea na wadau na wataalamu wa
kiswhali katika ukumbi wa Maendeleo na Ushirikiano wa Kimataifa ( MS
TCDC) wakati wa ufunguzi wa Tamasha la Kiswahili leo Jijini Arusha.
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa
na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akisoma maandishi
yaliyoandikwa katika mkeka ikiwa ndiyo kiashiria cha kufungua Tamasha la
Kiswahili leo Jijini Arusha.
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa
na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akionyesha ujumbe wa maandishi
uliwahi kusema na Baba wa taifa Hayati Julius Nyerere (Taifa lolote
lisilokuwa na Utamaduni wake ni Taifa Mfu) wakati wa ufunguzi wa Tamasha
la Kiswahili leo Jijini Arusha.
Kikundi cha Ngoma kikitoa burudani
kwa washiriki wa Tamasha la Kiswahili (hawapo katika picha) wakati wa
ufunguzi wa Tamasha hilo leo Jijini Arusha.
(Picha na Lorietha Laurence-WHUSM,Arusha).
………………..
Na Lorietha Laurence- WHUSM,Arusha
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe awapa kongole wadau na wataalamu wa
lugha ya Kiswahili nchini na nchi za jirani (Jumuiya ya Afrika ya
Mashariki) waliojitokeza kwa wingi kushiriki ufunguzi wa Tamasha la
Kiswahili Jijini Arusha.
Dkt. Mwakyembe ametoa pongezi hizo
leo Jijini hapo wakati wa ufunguzi wa tamasha hilo lililokuwa na kauli
mbiu ya “Tukienzi Kiswahili na Utamaduni kama nyenzo muhimu za
maendeleo” lengo ikiwa ni kuibidhaisha lugha hiyo katika sehemu
mbalimbali duniani.
“jukwaa hili ni fursa nzuri ya
kuhakikisha tunatoka na nia moja ya kuweza kuifikisha lugha yetu ya
Kiswahili katika maeneo mbalimbali duniani ili ifahamike na kutumika
kama lugha ya mawasiliano” Dkt. Mwakyembe.
Aidha aliongeza kwa kusema kuwa
tayari lugha ya Kiswahili imepiga hatua kubwa kwa upande wa Afrika
ambapo Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika imeipitisha
lugha hiyo kuwa miongoni mwa lugha nne rasmi za mawasiliano kwa
mwanachama hao.
“Hapa juzi katika mkutano wa wakuu
wa nchi wa Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini Mwa Afrika
uliofanyika tarehe 18 Agosti 2019 tumeshuhudia Kiswahili kimekubaliwa
kuwa moja ya lugha nne rasmi ya mawasiliano kwa jumuiya hiyo”
Anazidi kueleza kuwa azma ya Rais
wa awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli ni kuhakikisha lugha ya Kiswahili inabidhaishwa na kufanywa
kuwa chanzo muhimu cha ajira na mapato kwa wataalamu wa lugha hiyo
nchini na nje ya nchi.
Naye Katibu Mtendaji Baraza la
Kiswahili la Taifa (BAKITA) Dkt. Selemani Sewange ameeleza kuwa tamasha
hilo ni la kipekee kuandaliwa na Baraza lake ambapo mada mbalimbali
zitakazowasilishwa zenye lengo la kutoa elimu kwa umma kuhusu lugha ya
Kiswahili.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Bodi
wa Chuo Cha Maendeleo na Ushirikiano wa Kimataifa ( MS TCDC ) Dkt.
Servacius Likwelile aliwashukuru wadau , wataalamu na wote waliojitokeza
kufanikisha tamasha hilo .
Tamasha hilo limefanyika kwa mara
ya kwanza baada ya kusimama kwa muda wa miaka 12 , ambapo mara ya mwisho
lilifanyika mwaka 2007 kwa jina ya Siku ya Kiswahili .
No comments :
Post a Comment