Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza
jambo wakati wa uzinduzi wa kongamano linalohusisha wadau mbalimbali wa
masuala ya UKIMWI linaloendelea Jijini Arusha.
Naibu Waziri wa Afya Dkt.
Faustine Ndugulile akiangalia moja ya bidhaa zinazotengenezwa na kikundi
cha wajasiriamali waliokua wanatumia madawa ya kulevya kabla ya
ufunguzi wa kongamano la wadau mbalimbali wanaojihusisha na takwimu za
ugonjwa wa UKIMWI linaloendelea jijini Arusha.
Naibu Waziri wa Afya Dkt.
Faustine Ndugulile (wa tatu kulia) akijadiliana jambo na makamu
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma na maendeleo ya Jamii
Mhe. Juma Nkami (wa kwanza kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa NIMR prof.
Yunus Mgaya na wengineo baada ya kumaliza ufunguzi wa kongamano la wadau
mbalimbali wanaojihusisha na masuala ya tafiti za UKIMWI nchini
linaloendelea jijini Arusha.
Naibu Waziri wa Afya Dkt.
Faustine Ndugulile akiwa katika picha ya pamoja na washiriki mbalimbali
wanaohudhuria kongamano la wadau wanaohusika na masuala ya tafiti za
ugonjwa wa UKIMWI linaloendelea jijini Arusha.
Makamu Mwenyekiti wa kamati ya
kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Juma Nkamia
akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la wadau mbalimbali wa
masuala ya tafiti za ugonjwa wa UKIMWI linaloendelea Jijini Arusha.
Naibu Waziri wa Afya Dkt.
Faustine Ndugulile akiangalia moja ya bidhaa zinazotengenezwa na kikundi
cha watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI wakati alipotembelea mabanda
mbalimbali kabla hajafungua kongamano la wadau wa Masuala ya UKIMWI
linaloendelea Jijini Arusha.
……………………………………………..
Na WAJMW-ARUSHA
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile ametaka
maboresho ya mifumo ya takwimu za tafiti mbalimbali zinazofanyika
nchini.
Dkt. Ndugulile amesema hayo
wakati akizindua kongamano linalohusisha wadau mbalimbali
wa masuala ya
UKIMWI ambao wanawasilisha tafiti na takwimu mbalimbali ambazo
zinaendelea kufanyiwa kazi nchini.
“Tunahitaji tuboreshe mifumo yetu
ya takwimu ili tuwe na uwiano wa takwimu ambazo zinawasilishwa katika
mkutano huu, hapa nimeona takwimu mbalimbali zimewasilishwa, ninaomba
takwimu hizo ziwe za wote kwa sababu tuna wadau wengi wanaoshiriki
katika mapambano haya dhidi ya Ugonjwa wa UKIMWI hivyo maelekezo yangu
kuwe na mfumo mmoja wa takwimu ambao kila mmoja atakua anachangia
takwimu zake na mfumo huo uwe wa mwisho utakaotoa takwimu za wote”.
Amesema Dkt. Ndugulile.
Hata hivyo Dkt. Ndugulile
amehamashisha makongamano kama hayo yafanyike mara kwa mara ili
kuwawezesha wanazuoni, watunga sera na walengwa kukaa pamoja ili
kujadiliana mambo mbalimbali ambayo yanahusuana na afua ambazo
zinatekelezwa hapa nchini.
Kongamano hilo limeshirikisha
taasisi za Serikali ambazo ni NIMR na TACAIDS pamoja na wadau mbalimbali
wanaofanya tafiti kuhusiana na ugonjwa wa UKIMWI ambao wamekutana ili
kuwasilisha takwimu za tafiti mbalimbali ambazo wanazifanyia kazi katika
maeneo yao.
No comments :
Post a Comment