
Dr. Pepretua Kalimasi Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano ya Nje na Ushirikishwaji wa Jamii
(DELCE), akifungua mafunzo ya Maafisa kutoka Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI – Babati na Arusha) mkoani
Morogoro. Kushoto ni Dr. Daudi Pascal Ndaki, Mratibu wa mafunzo.

Baadhi ya washiriki wa Mafunzo
maalumu ya Uwekezaji Mkakati wakisikiliza kwa makini mafunzo
yanayoendelea chuoni Mzumbe Morogoro.

Mkufunzi Mkuu wa mafunzo ya
maafisa toka TAMISEMI Dr. Nelson Ngilangwa akijitambulisha kwa washiriki
(hawamo pichani). Kushoto ni Dr. Dr. Pepretua Kalimasi.

Baadhi ya Washiriki wakiwa katika majadiliano ya vikundi na wakufunzi wao.

Dr. Daudi Pascal Ndaki
akiwasilisha mada kwa washiriki wa mafunzo ya Uwekezaji Mkakakati
yanayoendelea Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi Kuu Morogoro.
………………….
Chuo Kikuu Mzumbe kupitia
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Nje na Ushirikishwaji wa Jamii (DELCE);
wanaendesha mafunzo mahsusi kwa Maafisa kutoka Ofisi ya Rais Tawala za
mikoa
na Serikali za Mitaa Babati na Arusha kuhusu namna bora ya
kuandaa Uwekezaji Mkakati wenye lengo la kuongeza utendaji wenye tija
katika kufikia malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano.
Akizungunza wakati wa ufunguzi
wa mafunzo hayo; Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi hiyo Dr. Perpetua
Kalimasi, amesema Chuo Kikuu Mzumbe kimejizatiti katika utoaji wa
mafunzo bora kuendana na mahitaji ya wadau. Kupitia wataalamu wake wa
ndani wameweza kubuni kozi mbalimbali za muda mfupi kuwezesha kuwajengea
uwezo na kuwapa ujuzi wataalamu katika sekta mbali mbali ili
kuhakikisha malengo ya jumla katika Serikali na Sekta binafsi
yanafikiwa.
“ Kama Chuo chenye dhamana ya
kutoa Elimu bora kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Nje na
Ushirikishwaji wa Jamii; tumebuni kozi nyingi fupi fupi kupitia
wataalamu wetu kuweza kufundisha makundi mbalimbali ya watumishi na
jamii kwa ujumla ili kuwawezesha kuleta ufanisi na kufikia malengo
kulingana na mipango ya kiutendaji waliyojiwekea; hususani katika
kipindi hiki ambacho Serikali ya Awamu ya Tano imewekeza katika Uchumi
wa Viwanda” alisema
Aidha amewataka washiriki
kutumia vema muda wa mafunzo waliojipangia kuhakikisha wanajifunza na
kupata ujuzi katika masuala yanayohusu “Uwekezaji Mkakati” ili mafunzo
hayo yawawezeshe kuleta mapinduzi katika shughuli wanazozisimia huku
akiwataka kuwa mabalozi wazuri katika kutangaza mafunzo mbalimbali
yanayotolewa na Chuo Kikuu Mzumbe kwa wadau mbali mbali nchini.
Naye mratibu wa mafunzo hayo
Dr. Daudi Pascal Ndaki amesema mafunzo hayo yamelenga kuhakikisha
wataalamu hao wanapata mafunzo ya nadharia na vitendo kupitia wataalamu
wabobevu na kwamba washiriki watakuwa na fursa nzuri ya kubadilishana
uzoefu na kutatua kwa pamoja changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza
katika maeneo yao ya kazi.
Aidha mafunzo hayo yatahusisha
mada mbalimbali zinazohusu Uwekezaji Mkakati, mbinu na mikakati ya
kuainisha maeneo ya uwekezaji hususani ile inayohusu utatuzi wa matatizo
ya jamii na namna ya kuandika miradi inayoweza kupata ufadhili wa ndani
na nje. Matokeo ya mafunzo hayo ni kuwa na wataalamu wenye uwezo wa
kuandika miradi ya maendeleo na uwezo wa kutafuta fedha za kuanzisha na
kuendesha miradi ya maendeleo katika maeneo yao ya kiutendaji.
No comments :
Post a Comment