Thursday, September 12, 2019

BENKI YA POSTA TAWI LA MOROGORO YATOA VIFAA TIBA KWA AJIRI. YA AJALI YA MOTO MOROGORO



Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Bi. Regina Chonjo akipokea vifaa tiba kutoka kwa meneja wa Benki ya Posta tawi la Morogoro Bi.Ulimwengu Mwangama kwa ajili ya kuwasaidia mjeruhi waliolazwa katika hospitari ya rufaa ya mkoa wa Morogoro waliopata ajali ya moto agosti kumi mwaka huu.
Baadhi ya vifaa  tiba vilivyotolewa na Benki ya Posta
NA FARIDA SAIDY, MOROGORO
MAJERUHI  Kumi na nane wa ajali ya moto iliyosababishwa na lori la mafuta kuwakamoto iliyotokea agosti Kumi mwaka huu eneo la msamvu manispaa ya morogoro ambao walikuwa
wamelazwa katika hospitali ya Rufaa mkoa w a Morogoro wanaendelea vizuri ambapo katiyao kumi nanne wameruhisiwa huku wane wakiendelea kupatiwa matibabu hospitalini hapo.
Akizungumza wakati wakipokea msaada wa vifaa tiba kutoka benki ya Posta  Mganga Mfawidhi wa hospitali ya rufaa mkoa wa Morogoro Dokta Rita Lyamuya amesema kuwa tangu kutokea kwa tukio hilo wamekuw wakishirikiana na madakatari kutoka ndani na nje ya mkoa Wa Morogoro ili kupigania uhai wa majeruhi hao hivyo hadisasa majeruhi kumi na nne wamepona na kuruhusiwa .
Bi.Ulimwengu Mwangama nimeneja wa benki ya Posta tawi la Morogoro amesema kufuatia tukio hilo wameguswa hivyo wamejitolea vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni tatu ili kusaidia majeruhi hao.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Morogoro Bi. Regina Chonjo ameishukuru taasisi hiyo na kutoawito kwa mashirika mengine kuendelea kutoa msaada kutokana na mkoa wa Morogoro kupitiwa na barabara kuu ziendazo mikoa ya kanda ya Ziwa ,Nyanda za juu kusini na nchi za nje huku mganga mkuu wa mkoa wa Morogoro Dokta Kusirye Ukio amewahakikishia kutumia vifaa hivyo kama vilivyokusiwa.
Katika ajali hiyo zaidi yawa tusabini wlipoteza maisha papohapo huku zaidi ya sabini kujeruhiwa.
nchi za nje huku mganga mkuu wa mkoa wa Morogoro Dokta Kusirye Ukio amewahakikishia kutumia vifaa hivyo kama vilivyokusiwa.
Katika ajali hiyo zaidi yawa tusabini wlipoteza maisha papohapo huku zaidi ya sabini kujeruhiwa.

No comments :

Post a Comment