![]() |
| Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, bunge, kazi, vijana, ajira na watu wenye ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akisalimiana na mmoja wa washiriki wa warsha hiyo Bi. Mariagorete Charles mara baada ya ufunguzi wa warsha hiyo Agosti 26, 2019. |
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, bunge, kazi, vijana, ajira na watu
wenye ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi
wa warsha ya siku moja ya majadiliano ya wadau kuhusu ushiriki wa
Watanzania katika miradi ya kimkakati (Local content) katika sekta ya
uziduaji mkoani Dodoma iliyofanyika tarehe 26 Agosti, 2019.

Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia sera, bunge, kazi,
vijana, ajira na watu wenye ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akiteta jambo na
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Bilinith Mahenge mara baada ya
kufungua warsha ya majadiliano ya wadau kuhusu ushiriki wa Watanzania
katika miradi ya kimkakati (Local content) katika sekta ya uziduaji
mkoani Dodoma.

Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Bilinith Mahenge pamoja na sehemu ya
washiriki wa warsha hiyo wakifuatilia mada kutoka kwa mwezeshaji Bi.
Mariagorete Charles kutoka katika mradi wa EACOP (hayupo pichani) wakati
wa warsha hiyo.

Sehemu
ya washiriki wa warsha hiyo wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu (Sera, bunge, kazi, vijana, ajira na watu wenye ulemavu)
Mhe.Jenista Mhagama (hayupo pichani) alipokuwa akitoa hotuba yake wakati
wa ufunguzi wa warsha hiyo.

Mwasilishaji
wa mada kuhusu mradi ya bomba la mafuta – EACOP Bi. Mariagorete Charles
akiwasilisha mada wakati wa warsha hiyo kwa washiriki wa warsha
iliyofanyika Agosti 26, 2019 Jijini Dodoma.

Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia sera, bunge, kazi,
vijana, ajira na watu wenye ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akizungumza
jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Bilinith Mahenge
*****************
NA.MWANDISHI WETU
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi,
Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama amefungua warsha
ya siku moja ya majadiliano ya wadau kuhusu ushiriki wa Watanzania
(Local content) katika sekta ya uziduaji mkoani Dodoma.
Warsha
hiyo imewakutanisha pamoja wawakilishi zaidi ya 100 wa makundi
mbalimbali kutoka Wilaya zote za Mkoa wa Dodoma ili kujadili mikakati na
maendeleo ya utekelezaji wa dhana ya ushiriki wa Watanzania katika
fursa za miradi ya kimkakati ikiwemo mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la
Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Hoima nchini Uganda kwenda Tanga,
Tanzania na sekta ya madini kwa ujumla.
Akizungumza
wakati wa kufungua warsha hiyo leo Agosti 26, 2019 katika ukumbi wa
Kilimanjaro Hazina Mjini Dodoma Waziri Mhagama aliwataka viongozi wa
maeneo ambako bomba litapita wawahamasishe wananchi kuchangamkia fursa
zitakazokuwepo katika utekelezaji wa mradi huo na kujiletea maendeleo.
“Ni
wakati sahihi sasa kuitumia fursa hii ya miradi mikubwa ambayo inalenga
kunufaisha wananchi kwa kuzingatia kuwa ajira zitazalishwa kwa wazawa
hivyo mjiandaae kikamilifu katika kuupokea mradi huu,” alieleza Mhagama.
Waziri
Mhagama aliongezea kuwa, Sheria ya Mafuta imeweka wazi kwamba
watanzania na kampuni za kitanzania zinatakiwa zipewe kipaumbele wakati
wa ununuzi. Serikali inaamini kwamba Sekta binafsi ina mchango mkubwa
katika kuinua uchumi wa nchi. Hivyo ni matarajio kwamba Mkandarasi wa
mradi atazingatia matakwa ya Sheria hii na pale ambapo kampuni za
kitanzania hazina uwezo basi ziingie ubia na kampuni za nje ili kuongeza
ujuzi wa uzalishaji na utoaji wa huduma.
Alifafanua
kuwa, kwa kuzingatia dhamira ya Serikali ya awamu ya Tano kuona
Watanzania wanamiliki uchumi wao, hivyo wataendelea kuwahamasisha
watanzania kushiriki katika miradi Mikubwa ya kimkakati na katika
miradi mbalimbali.
“Serikali
kupitia Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchu Kiuchumi imejipanga
kuweka mazingira wezeshi kwa watanzania ikiwa ni pamoja na kutengeneza
Sera na Sheria na miongozo inayotoa kipaumbele kwa watanzania kupata
fursa za ajira, kushiriki kwa kutoa huduma, uuzaji wa bidhaa na utoaji
wa huduma kwenye miradi inayotekelezwa hapa nchini hasa katika sekta ya
uziduaji,”alisisitiza Mhagama.
Mradi
wa EACOP ni moja kati ya miradi mikubwa ambao una manufaa mengi kwa
nchi yetu na kueleza kuwa, bomba hili la mafuta ghafi litakuwa na urefu
wa km 1443 kati ya hizo km 296 zitakuwa nchini Uganda na km 1147
zitakuwa Tanzania. Hii ni fursa kubwa kwa watanzania kwa kuwa 80% ya
mradi huu utapita Tanzania.
Aidha
alibainisha mikoa itakayopitiwa na mradi huo ikiwemo Kagera, Geita,
Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Manyara na Tanga na kufafanua kuwa
bomba hilo litapita katika wilaya 24, Kata 134 na vijiji zaidi ya 180 na
kutoa wito kwa wananchi kujiandaa na kuhakikisha wanaandaa mazingira
wezeshi katika kushiriki fursa zitakazotokana na uwepo wa mradi huo.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Bilinith Mahenge
alipongeza jitihada zinazoendelea katika kuhamasisha na kutoa elimu kwa
jamii juu ya ushiriki wa Watanzaia katika fursa ya mradi bomba la mafuta
na kuahidi kuzimamia kikamilifu ili kuhakikisha jamii inashiriki kwa
uhakika.
“Kipekee
ninapongeza juhudi zinazoendelea katika kuhakikisha wananchi
wanajikwamua kiuchumi kwa kuzingatia ujio wa miradi hii ya kimkakati
nchini hivyo hatuna budi kuendelea kutoa rai kwa Watanzania wote
kuchangamkia fursa hizi,”alisema Dkt. Mahenge.


No comments :
Post a Comment