Mgeni rasmi wa kongamano la Malkia wa nguvu na muigizaji wa filamu nchini Hidaya Njaidi
akiangalia
bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na wanawake katika njanja mbalimbali
wakati wa kongamano hilo, leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
na mwandaaji wa umoja wa Malkia wa Nguvu,Grace Mpanduka (kulia)
akizungumza na baadhi wa waandishi wa habari mara baada ya kufungua
kongamano maalum la wanawake la malkia wa nguvu , ambapo amewashauri wanawake kuchangamkia fursa za kiuchumi zilizopo ili kujikwamua kiuchumi, leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa taasisi ya Nafanikiwa Inspiration,Reuben Ndimbo(katikati) akizungumza na waandishi wa habari katika kongamano la maalum la wanawake la malkia wa nguvu ambapo amewashauri wananchi kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya tano katika ujenzi wa uchumi, leo jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi na muigizaji wa filamu nchini Hidaya Njaidi akiwasili
katika ukumbi wa TGNP uliopo Mabibo jijini Dar es Salaam ili kuendelea
na shughuli ya kongamano la Malkia wa nguvu
WANANCHI
kote nchini hasa wanawake wameshauriwa na kutakiwa kuchangamkia fursa
za kiuchumi zilizopo ili kuweza kujiongezea kipato binafsi na
kuondokana na umaskini.
Akizungumza
katika kongamano maalum la wanawake la malkia wa nguvu lililofanyika
leo jijini Dar es Salaam mwenyekiti wa taasisi isiyo ya serikali ya
Nafanikiwa Inspiration Reuben Ndimbo amesema kuwa kuna kila aina ya
fursa nchini ambayo ikitumiwa vyema itaeleta matunda, hivyo watanzania
wanatakiwa kuzichangamkia ili ziweze kuwanufaisha wao binafsi na taifa
kwa ujumla.
Aidha
ameongeza kuwa kutokana na kasi ya serikali ya awamu ya tano chini ya
Rais Dkt. John Joseph Magufuli kufungua ya uwekezaji katika sekta ya
viwanda ni vyema sasa kila mwenye nafasi kuwekeza katika viwanda
vidogo, vya kati na vikubwa.
Kwa
upande wake muandaaji na mwenyekiti wa umoja wa Malkia wa nguvu, Grace
Mpanduka amesema kuwa wanawake ni walengwa wakubwa katika kongamano
hilo kutokana na uchakalikaji wao wa na wanaaminika katika kuchangamkia
na kuzitendea kazi fursa zinazopatikana hapa nchini.
Amesema
kuwa nafasi ya uenyekiti wa SADC kwa Rais Dkt John Joseph Magufuli ni
fursa kubwa sana kwa watanzania na hatuna budi kuongeza ubunifu katika
nyanja mbalimbali ikiwemo nyanja za utalii, na ubunifu katika mambo
mengine mengi.
“Mimi
nimejitolea kuwafungua na kuwaelimisha watanzania wenzangu hasa akina
mama ili wafahamu nchi za wenzetu wanavyochangamkia fursa kama hizi
pindi zinapotokea katika nchi zao, mwaka huu mmoja wa uenyekiti wa Rais
Magufuli katika nchi za SADC ulete mabadiliko nchini” Amesema.
Aidha
amempongeza Rais Magufuli kwa uchapakazi na ufunguaji milango ya fursa
kwa wanawake kwa kuwataka kuchapa kazi kwa kuanzisha viwanda na
biashara zingine zitakazo itangaza nchi yetu katika mataifa ya nje.
Pia
amewaomba wanawake kutumia nafasi ya SADC kufungua milango kwa kwenda
nje ya nchi kujifunza jinsi wenzetu wanavyochangamkia fursa kama za
namna hiyo pamoja na ubunifu wanaotumia katika kufanya biashara.
No comments :
Post a Comment