Rais Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia Mkutano wa Sita
Jukwaa la Uongozi la Afrika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulujijini Dar es salaam leo Agosti 20, 2019
Jukwaa la Uongozi la Afrika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulujijini Dar es salaam leo Agosti 20, 2019
RAIS
Dk. John Magufuli, ametaja mambo sita zinazoifanya Afrika iendelee kuwa
maskini na kutawaliwa na wakoloni mbali ya utawala wa kikoloni kukoma
miaka zaidi ya 50 iliyopita.
Alisema hayo jana ikulu jijini Dar es Salaam katika mkutano wa sita wa jukwaa la viongozi barani Afrika (6th
African Leadership Forum), ambapo ulikutanisha maraisa sita wastaafu wa
Afrika kujadili masuala mbalimbali yanayoifanya Afrika kubaki nyuma.
Kaulimbiu ya mwaka huu inasema: Kukuza Usimamizi mzuri wa Rasilimali za Asili kwa Mabadiliko ya Kijamii na kiuchumi barani Afrika,
ambapo kikubwa ni kuangalia namna viongozi wanavyosimamia rasilimali za
asili kwa ajili ya mabadiliko ya kiuchumi barani Afrika.
Akitaja sababu hizo Rais Magufuli
alisema, kwanza ni kuwepo na masalia ya fikra za ukoloni. Kuhusu sababu
hii alibainisha bado kuna viongozi wa kiafrika wanafikiria kutawaliwa
badala ya kujitawala.
“Kama hujitegemei huwezi kuwa
huru, watu waliotutawala hawawezi kuwa wasaidizi wetu, lazima tuondokane
na fikra za kikoloni tuanze kujiamini kama tunaweza kama waafrika,
tukisimama pamoja naamini tutafanya makubwa,” alisema Rais Magufuli.
Sababu ya pili alisema ni
kushindwa kusimamia rasilimali za Afrika, ambapo katika hili alisema
wengi wanaamini fedha ndio msingi wa maendeleo kitu ambacho si kweli.
“Mwalimu Julius Nyerere aliwahi
kutaja sababu tatu za kuendelea, alisema ili tuendelee lazima tuwe na
watu, siasa safi na uongozi bora. Hakutaja mahali popote kama fedha ni
msingi wa maendeleo.
“Akili zetu tumezielekeza kwenye
mikopo na misaada, hakuna mjomba kutoka nje atakayekuja kutusaidia,
tunazo rasilimali zalima tuzitumie vizuri halafu pesa zenyewe zitakuja,”
alisema.
Aidha, sababu ya tatu ya kuifanya
Afrika ibaki kuwa masikini Rais Magufuli alisema ni ukosefu wa ubunifu
katika masuala ya tekonolojia na uanzishwaji viwanda.
Alibainisha, malighafi nyingi za
bidhaa zinazouzwa katika soko la dunia zinatoka barani Afrika, lakini
viongozi wamekosa uthubutu katika ubunifu na teknolojia ya viwanda.
Sababu ya nne ni migogoro na hali
tete ya kisiasa barani Afrika, ambapo watu wanatumia muda mwingi
kufanya siasa badala ya shughuli za kimaendeleo. Matokeo yake kunakuwa
na vurugu zinazorudisha nyuma shughuli za kimaendeleo.
“Maeneo mengi yenye rasilimali
kuna migogoro, tunafahamu migogoro hii inaanzishwa na mabeberu kwa
kushirikiana na vibaraka wao waliopo barani Afrika. Wakati nchi zipo
kwenye vurugu wao wanavuna rasilimali zetu wanatuachia mashimo,”
alisema.
Sababu ya tano aliitaja ni
mikataba mibovu inayosababisha kuchukuliwa kwa rasilimali za Afrika.
Ambapo, viongozi wasio waaminifu wamekuwa wakishirikiana na mabeberu
kuchota rasilimali za Afrika kwa kutumia mikataba isiyozingatia pande
mbili za makubaliano.
“Mikataba mingi ilikuwa
inasimamia upande mmoja, mmoja ananufaika na mwingine anaumia. Hii yote
imesababishwa na ukosefu wa uzalendo, mabebertu na vibaraka wao
wanawahadaa wananchi na kuchukua rasilimali zao, wao wanaangalia matumbo
yao lakini wanaoumia na vizazi vijavyo,” alibainisha.
Katika mlolongo wake, Rais
Magufuli aliitaja sababu ya tano kuwa ni uharibifgu wa mazingira na
maliasili zilizopo barani Afrika ambazo hazipatikani kwengineko.
Alisisitiza, uharibifu wa
mazingira unaofanyika kwa kukata miti hovyo ili kuitumia kwa nishati ya
mkaa kunasababisha ukame, mafuriko na mmommonyoko wa ardhi.
“Yote hii inasababishwa na
ukosefu wa nishati ya uhakika ya kutumia majumbani, lakini tumeamua
kuondoa tatizo hili kwa kushirikiana kwa pamoja kama nchi za Kiafrika
ili kuacha utegemezi,” alisema Rais Magufuli.
No comments :
Post a Comment