Meneja
Ugavi wa TBL, Poul Canute akikabidhi vifaa vilivyotolewa na wafanyakazi
kwa Afisa Mwandamizi kutoka taasisi ya Her Africa, Asnath Ndosi Wakati
wa hafla hiyo,wengine pichani ni wafanyakazi wa TBL
Meneja wa masuala Endelevu wa TBL,Irene Mutiganzi (wa tatu kushoto) Akiongea Wakati wa hafla hiyo.
Maofisa
wa taasisi ya Her Africa wakifurahia msaada huo wa kusaidia wasichana
kukabiliana na changamoto ya hedhi wakati wa hafla hiyo.
Baadhi
ya wafanyakazi wa TBL wakifuatilia matukio wakati wa hafla hiyo.
Na Cathbert kajuna - Kajunason/MMG.
Wafanyakazi wa kampuni yak Bia Tanzania (TBL Group), chini ya kampuni
mama ya kimataifa ya AB InBev, wametoa msaada wa taulo za kike kwa ajili
ya kuwasitiri wasichana wanafunzi wanaosoma shule za sekondari kupitia
mradi wa kukabiliana na changamoto za hedhi unaoendeshwa na taasisi ya
Her Africa.
Hafla ya kukabidhi msaada huo ilifanyika katika ofisi za makao makuu ya
TBL zilizopo Ilala jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wafanyakazi
maofisa kutoka taasisi ya Her Africa na wafanyakazi wa TBL.
Akiongea wakati wa hafla hiyo, Meneja wa Masuala Endelevu wa TBL, Irene
Mutiganzi, alisema kuwa msaada huo umetolewa kutokana na michango ya
wafanyakazi baada ya kuguswa na changamoto ya vifaa vya hedhi
mashuleni kwa wasichana, hususani wanaotoka kwenye familia zenye vipato
vidogo na kuwapunguzia uwezo wao wa kufaulu vizuri kutokana na wengine
kutohudhuria masomo wanapokuwa kwenye vipindi hivyo.
“TBL tunayo sera ya kujenga ulimwengu maridhawa ambayo inatekelezwa pia
na wafanyakazi, ambapo mara nyingi wamekuwa wakijitoa kukabiliana na
changamoto za kijamii na sio kwa kutoa pesa tu bali pia wamekuwa wakitoa
hata muda wao kushiriki katika kazi za kijamii kama ambavyo
wamefanikisha kutoa mchango huu” alisema Mutiganzi.
Kwa upande wake Mwanzilishi mwenza wa taasisi ya Her Africa nchini,
Salha Kibwana, alishukuru wafanyakazi wa TBL kwa kulipa kuipa umuhimu
changamoto ya vifaa vya Watoto wa kike wa sekondari kujisitiri
wanapokuwa kwenye vipindi vya hedhi mashuleni, kwa kutoa msaada huo na
amewahakikishia kuwa utawafikia walengwa “Nawashukuru kwa kujitoa na
nina imani tukizidi kuunganisha nguvu tutafanikiwa kusaidia wanafunzi
wengi zaidi hususani maeneo ya vijijini” alisema
No comments :
Post a Comment