
Mwasilishajiwa wa sehemu 6-8 ya
Sheria namba 5 ya mwaka 2018 Fatma Gharib Haji akiwasilisha mada kwa
wajumbe waliyofika katika Mkutano wa kujenga uwelewa wa sheria ya
ushindani halali wa biashara na kumlinda mteja (katikati) ni Ummy
Mohamed Rajab Mwasilishaji wa sehemu 4-5 na wa kwanza kushoto Mkuu wa
Kitengo cha Muungano ya Makampuni na Udhibiti wa Ushindani (ZFCC).
Mmanga Khamis Machano.

Afisa Mwandamizi Ushauri wa
Ushindani kutoka Tanzania bar akitoa Maelezo kwa wadau waliyoshiriki
katika mkutanowa kujenga uwelewa wa sharia ya ushindani halali wa
biashara na kumlinda mteja katika ghafla iliyofanyika Ukumbi wa Makonyo
Pemba.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya
Ushindani Mohamed Jafari Jumanne akitoa ufafanuzi wa kujenga uwelewa wa
sheria ya ushindani halali wa biashara na kumlinda mteja ghafla hiyo
imefanyika katika Ukumbi wa Makonyo Pemba.

Wakili wa Serikali kutoka Afisi ya
Mkurugenzi wa Mashtaka Asia Ibrahim Mo’hd akitoa ushauri kwa
wawasilishaji kuwapatia elimu wafanya bishara na wanunuzi katika mkutano
wa kuwajengea uwelewa wa sharia ya ushindani halali wa biashara na
kumlinda mteja katika ukumbiwa wa Makonyo Pemba.

Mohammed Ali Maalim ambaye ni
mjumbe aliyeshiriki katika mkutano wa kuwajengea uwelewa wa sharia ya
ushindani halali wa biashara na kumlinda mteja akitoa ushauri kwa
wafanya bishara kujilinada katika kaizi zao ghafla hiyo imefanyika
katika ukumbi wa Makonyo Kisiwani Pemba.

Wajumbe mmbalimbali waliyoshiriki
katika mafunzo ya mkutano wa kuwajengea uwelewa wa sharia ya ushindani
halali wa biashara na kumlinda mtumiaji wakichukuwa wakifuwatilia
mkutano huouliyofanyika katika ukumbi wa Makonyo Kisiwani Pemba.
Picha na Miza Othman –Maelezo.
………………………
HASINA KHAMIS ,MAELEZO- PEMBA.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya
Ushindani halali wa biashara na kumlinda mtumiaji, Mohamed Jafari
Jumanne aliwataka wafanya biashara kuwa mabalozi kwa wenzao kwani
wafanyabiashara wengi wanakimbilia kuekeza katika nchi ambazo hazina
tume ya ushindani ili kuwarahisisha kuingiza bidhaa bandia.
Hivyo aliwataka wafanya biashara
hao kujiorodhesha katika Tume ya ushindani ili kuweza kuepuka kuingiza
bidha bandia pamoja na matumizi ya nembo zisizo rasmi.
Hayo aliyasema wakati akifungua
mafunzo ya kujenga uwelewa wa Sheria ya ushindani halali wa biashara na
kumlinda mteja ya Sheria nambari 5 ya Mwaka 2018 ,huko katika Ukumbi wa
Makonyo Chake Chake Pemba.
“Miongoni wa umuhimu wa sheria
hiyo ya nambari 5 kwa wananchi ni kujua haki zao katika biashara pamoja
na kuzuia uingizaji ,uzalishaji wa bidhaa bandia ndani na nje ya
Nchi”alieleza.
Aidha Mkurungezi huyo alisema Tume
inajitahidi kupambana na bidhaa hizo za bandia zinazoingizwa ikiwemo na
wale wafanyabiashara ambao wanatumia nembo za Kampuni nyengine kuvutia
wateja .
Pia aliwatoa hofu wananchi juu ya
Mchele wa Mapembe ambao ndio chakula kikubwa watumiacho Wananchi wa
Visiwa hivi kuwa Mchele unapoingizwa katika Nchi ni lazima kupimwa na
kuchunguzwa usalama wa mlaji .
Alisema “wito wangu kwa
Wafanyabiashara kuhifadhi bidhaa zao katika sehemu salama ili kuepuka
uharibifu kwa bidhaa na kuweza kuleta matatizo kwa Wananchi”.
Hata hivyo alisema viko vitengo
mbali mbali vya ukaguzi ambavyo vinapita kila sehemu kukagua bidhaa
ambazo zimekwisha muda wake pamoja usalama wa watumiaji.
Pia Mkurugenzi hiyo wa Tume ya
ushindani ametoa tahadhari pale panapotokea sadaka ama kutolewa vitu
bure ,alisema ni vyema vitu hivyo vikachunguzwa kwanza .
“Ninawaomba Wakuu wa Wilaya ,Mikoa
,Masheha na Watu wengine kuwa waangalifu na bidhaa zinazotolewa kama
msaada pamoja na kwenda sehemu husika kutoa taarifa ya msaada huo ili
kuweza kupimwa na kuchunguza kwa ajili ya maslahi ya
wananchi”alisisitiza.
Akiwasilisha Mada ya sheria
nambari 5, Fatma Gharib Haji ,alisema sheria hiyo ina lengo mzuri kwa
Wananchi na wafanyabiashara ikiwemo kuwalinda na kuondoa changamoto za
Wafanyabiashara wa ndani na nje katika Soko la ushindani.
Nae Afisa Mwandamizi ushawishi wa
ushindani kutoka Tanzania bara, Alex Mmbaga nchi nyingi za jumuiya ya
maendeleo ya kusini wa Afrika SADC zimejikita katiksa suala la ushindani
katika biashara zao.
“Hivyo ni vyema wafanyabiashara wa
Zanzibar kuitumia tume hiyo kwa kukuza na kulinda biashara zao kwani
tume hiyo ina faida nyingi kwao na wananchi”alieleza.
Kwa upande wao washirika katika
mafunzo hayo walisema wameyapokea vyema mafunzo hayo na watakuwa
mabalozi kwa wenziwao ili kuona Tume ya ushindani wanaiunga mkono kwa
maslahi yao na wananchi
Mafunzo hayo yaliwashirikisha
Wafanyabiashara ,Wanunuzi ,Wanasheria ,Vyombo vya ulinzi na usalama
ikiwa na lengo la kuiweka wazi Sheria nambari 5 ya Mwaka 2018 ya tume ya
ushindani halali wa biashara na kumlinda mtumiaj
No comments :
Post a Comment