Katibu
Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Profesa Joseph Buchweishaija
amewataka watanzania wote kujitokeza kwa wingi kushiriki katika
maadhimisho na maonyesho ya nne ya wiki ya Viwanda ya Jumuia ya
Maendeleo ya Kusini mwa Africa (SADC) .
Maadhimisho
na Maonesho hayo yatafanyika kuanzia tarehe 5 hadi 8 Agosti 2019 katika
Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC); Viwanja
vya Karimjee na Gymkhana jijini Dar es Salaam.
Profesa Bucheishaija amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na
Biashara inawaalika wananchi kufika kwa wingi kwani tunatarajia jumla ya
nchi 15 wanachama wa SADC zitashiriki,
Aidha, ameongeza kuwa wiki hii ya SADC itawawezesha wananchi kuona fursa
mbalimbali ikiwemo kuweza kupata malighafi za kilimo ambazo viwanda
utumia kuzalisha bidhaa za viwandani. Miongoni mwa faida watakazozipata
watanzania kupitia maonesho ya Viwanda kwa nchi za Kusini mwa Afrika ni
pamoja na kujifunza au kubadilishana uzoefu na nchi nyingine za SADC
ambazo zitashiriki katika maonesho hayo pamoja na kuongeza wigo wa
masoko ya ndani na nje ya nchi.
Nafasi
imetolewa kwa kila mtanzania kujisajiri bado ipo mpaka tarehe 2 August,
2019 na wale ambao watakuwa hawajajisajiri wasiwe na wasiwasi maana
nao watatembelea maeneo ya maonesho kama wengine na kuweza kuona bidhaa
za nchi nyinyine, hivyo watu wote wanakaribishwa sana kwa ajili ya tukio
la kihistoria ambalo kutokea tena mpaka ipite miaka kumi na mitano.
Naye
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara ndugu Ludovick
Nduhiye ametoa ufafanuzi kuwa lengo kuu ni kuweka utayari kwa wananchi
hususani kwa Tanzania kuweza kushiriki kwa wingi na kuweza kujionea
fursa lukuki ambazo zitaonekana katika maoshesho hayo.
Aidha
bwana Nduhiye amewakaribisha wananchi kufika kwa wingi lengo likiwa
ni kuangailia fursa muhimu zitakazopatikana kwenye wiki hiyo ya
viwanda ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa masoko pamoja na ubadilishaji
wa mawazo namna ya kuanzisha viwanda mbalimbali pamoja na kupata fursa
mbalimbali kwenye nchi hizo za SADC.
Mwenyekiti
wa Kamati ya maandalizi ya maonesho na maadhimisho ya Wiki ya Viwanda
kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara bwana Ally Gugu ambaye ni
Mkurugenzi wa Idara ya Mtengamano na Biashara amewahimiza wananchi
kujisajili kupitia anuani zinazopatikana katika tovuti ya Wizara ya
Viwanda na Biashara ambayo ni www.mit.go.tz na kisha kubofya katika
linki mbili za haraka (quick link) ambazo ni Usajili Wiki ya Viwanda na
Usajili Mkutano wa 39 wa SADC.
Gugu
aliongezea kuwa haya maonesho ya viwanda ni fursa ya watanzania wote
kuanzia wajasiriamali wadogo, wajasiriamali wa kati pamoja na wenye
viwanda vikubwa ili tuweze kutimiza azima ya Serikali ya awamu ya tano
inayosisitiza maendeleo kupitia uchumi wa Viwanda ili Tanzania iweze
kufikia uchumi wa kati.
No comments :
Post a Comment