Wahamasishaji kutoka Jeshi la
Polisi wakishangilia timu ya Jeshi la Polisi ikiwa inacheza mpira wa
miguu na timu ya Polisi Burundi ambapo Tanzania iliibuka mshindi kwa
kuifunga Burundi bagoli 2 kwa 1.
Mwanariadha wa Polisi Tanzania
katika mbio za nyika WP. Catherine akiwa katika mbio hizo katika viwanja
vya Chuo Kikuu cha Kenyata jijini Nairobi, nchini Kenya ambaye
ameiwezesha nchi ya Tanzania kuingia katika nafasi ya pili katika
mashindano ya michezo ya EAPCCO 2019.
Mwanariadha wa Polisi Tanzania PC
Michael baada ya kumaliza mbio za mita 100 katika viwanja vya Kasarani
jijini Nairobi, nchini Kenya na kuiwezesha nchi ya Tanzania kuingia
katika nafasi ya pili katika mashindano ya michezo ya EAPCCO 2019.
…………………
Timu za Jeshi la Polisi Tanzania
zinazoshiriki katika michezo ya Wakuu wa Majeshi ya Polisi kwa nchi za
Kanda ya Afrika Mashariki (EAPCCO 2019) inayochezwa katika viwanja vya
Kasarani na Chuo Kikuu cha Kenyata, jijini Nairobi nchini Kenya
zimefanikiwa kupata jumla ya Medali 29. Katika medali hizo dhahabu 2,
Silva 7 pamoja na Medali 20 za Shaba.
Medali hizo zimepatikana katika
michezo mbalimbali ikiwemo, Judo, Taekwondo, Kareti, mchezo wa kurusha
vishale, Riadha, mchezo wa Kurusha kisahani, kuruka vihunzi, mpira wa
miguu, mpira wa kikabu, kulenga shabaha, kuvuta kamba pamoja na mpira wa
wavu.
Katika mchezo wa Taekwondo
mchezaji wa Tanzania Omary Ramadhani ambaye pia ni Mkufunzi katika
Shule ya Polisi Moshi (TPS) aliibuka mshindi kwa kumpiga Mkenya na
kufanikiwa kuingia fainali.
Aidha, katika michezo ya mbio za
nyika, Timu ya Kenya imeshika nafasi ya kwanza, Tanzania imeshika nafasi
ya mbili, Uganda nafasi ya tatu ambapo Sudani ya kusini ikishika mkia
kwa kupata nafasi ya nne.
Michezo hiyo ya Wakuu wa Majeshi
ya Polisi kwa nchi za kanda ya Afrika Mashariki (EAPCCO 2019)
inajumuisha nchi 14 ambapo kati ya hizo nchi 7 zipo katika mashindano
hayo. Nchi hizo ni Tanzania, Uganda, Rwanda, Burundi, Sudani, Sudani ya
Kusini pamoja na nchi ya Kenya ambayo ndio mwenyeji wa michezo hiyo.
Michezo hiyo ya EAPCCO 2019
ilifunguliwa na Waziri wa Usalama wa Ndani, Dkt. Fred Matiangi katika
viwanja vya Kasarani jijini Nairobi nchini Kenya ambapo aliwataka nchi
washiriki wa michezo ya EAPCCO kuimarisha ushirikiano, uhusiano pamoja
na kupanua wigo wa mawasiliano miongoni mwa nchi wanachama ikiwa ndio
lengo kubwa la muungano huo.
Dkt. Mataiangi amewahimiza nchi
wanachama wa EAPCCO kujikita katika kutekeleza mikakati ya kupambana na
uhalifu kwa kubadilisha uzoefu na taaarifa za kiitelijensi kikanda.
Pia, alisisitiza kuwa mikakati
hiyo itoe kipao mbele katika kubaini, kuzuia, kupambana na kupeleleza
makosa yanayovuka mipaka kama vile uhalifu wa kimtandao, usafirishaji
haramu wa binadamu, wizi wa magari pamoja na uhalifu wa mazingira.
Michezo hiyo ya Wakuu wa Majeshi
ya Polisi kwa nchi za Kanda ya Afrika Mashariki (EAPCCO 2019) imeingia
siku ya nne tangu kufunguliwa ambapo inatarajiwa kufikiwa kilele chake
septemba 2, 2019.
No comments :
Post a Comment