![]() |
| Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara yake kutembelea miradi inayosimamiwa na DAWASA na kuzungumzia hatua mbalimbali ilipofikia na kuwaondoa hofu wakazi wa maeneo ya Mkuranga baada ya kukaa bila maji safi kwa kipindi kirefu. |
Mwenyekiti
wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka DAWASA Jenerali Mstaafu
Davis Mwamunyange akiangalia mafundi wa DAWASA wakiwa wanaunganisha
mabomba kabla ya kuyalaza, ziara ya Mwenyekiti wa Bodi ilikua sambamba
na wajumbe pamoja Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian
Luhemeja.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumzia mradi wa
maji wa Mkuranga wenye thamani ya Bilion 5.5 unaotarajia kukamilika
ndani ya miezi nane kuanzia sasa na utahudumia wananchi 25,000 ambapo
maji yatasambazwa katika Vitongoji mbalimbali vya Wilaya ya Mkuranga.
Msimamizi
wa mradi wa maji Mkuranga kutoka DAWASA, Mhandisi John
Kirecha akielezea ramani ya mradi wa Maji Mkuranga kuanzia kwenye chanzo
cha maji Kulungu kuelekea kwenye tanki la maji la ujazo wa Lita Milioni
1.5 leo wakati wa ziara ya mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA Jenerali
Mstaafu Davis Mwamunyange pamoja na wajumbe wa bodi hiyo.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka DAWASA Jenerali Mstaafu
Davis Mwamunyange akiyajaribu maji kwa kuyaonja kutoka kwenye kisima
kilichopo Mkuranga kitakachohudumia wakazi wa maeneo hayo.
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Hayo
ameyasema wakati wa ziara yake katika mradi wa maji wa Mkuranga
ulioanza kutekelezwa hivi karibuni ukiwa umefikia kwenye hatua ya ujenzi
wa tanki la maji na ulazaji wa mabomba.
Mwamunyange
amesema, kulikuwa na changamoto zilijitokeza katika mradi huo ila kwa
sasa zimeshapatiwa ufumbuzi na wakandarasi wameshaingia kazini.
“Napenda
kusema hakuna udanganyifu katika mradi wa Mkuranga ila kulikuwa na
changamoto zilijitokeza na kwa sasa zimeshapatiwa uchambuzi na
wakandarasi wameingia kazini kuendelea na kazi,”amesema Mwamunyange.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema mradi huu ni
moja kati ya miradi sita iliyosainiwa hivi karibuni ukiwa na thamani ya
Bilion 5.5 na inatarajia kukamilika ndani ya miezi nane kuanzia sasa.
Luhemeja
amesema, kukamilika kwa mradi huu utahudumia wananchi 25,000 ambapo
maji yatasambazwa katika Vitongoji mbalimbali vya Wilaya ya Mkuranga.
“Katika
mradi huu kutakuwa na ujenzi wa tanki la maji lenye ujazo wa Lita
Milion 1.5 ambapo litasambaza maji katika maeneo mbalimbali na zoezi la
ulazaji wa mabomba linaendelea kwa sasa na wameangalia ubora wa mitaro
kwa kuchimba urefu wa mita 1.5 na mabomba yote ni mapya.
"Hatutarajii
kuona kuna changamoto ya upotevu wa maji katika mradi huu, kwani
mabomba yote ni mapya pia tumeangalia ubora wa mitaro kwa kuchimba mita
1.5 kwenda chini na utakamailika ndani ya muda wa miezi nane tokea
sasa,"amesema.
Msimamizi
wa mradi huo kutoka DAWASA, Mhandisi John Kirecha ameweka wazi kuwa
wameweza kufuata taratibu mbalimbali za kitaalamu kabla ya kuendelea na
ujenzi ambapo walichukua sampo ya mchanga eneo la ujenzi wa tanki na
kupeleka DIT na wakapata ushauri wa kuchimba urefu wa Mita 2.5 kwenda
chini.
Pia,
ameeleza kuwa watafunga Booster itakayosaidia kusafirisha maji kwa kasi
kuelekea kwenye tanki la maji la Mwanambaya lenye ujazo wa Lita 100,000
litakalotumika kama tanki la akiba ( reserve).
Mradi
wa Mkuranga unatarajiwa kukamilika mapema 2020, na utahudumia Mkuranga
na vitongoji vyake, maeneo ya Viwanda Kisemvule, Vikindu na wananchi wa
maeneo hayo wamefurahi kuja kwa mradi huo kutoka chanzo cha Maji Kulungu
ambapo wamekaa na shauku ya kupata maji safi na salama kwa muda mrefu.








No comments :
Post a Comment