Naibu Waziri, Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary
Mwanjelwa (Mb) akisisitiza uhifadhi mzuri wa nyaraka alipotembelea maktaba ya
Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dar es Salaam na kushuhudia
baadhi ya watafiti wakipata huduma ya taarifa zitakazowawezesha kukamilisha tafiti
zao.
Naibu Waziri, Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary
Mwanjelwa (Mb) akishuhudia baadhi ya nyaraka za Waasisi wa Taifa zilizotunzwa
katika maktaba ya Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa jijini Dar es Salaam
wakati wa ziara yake ya kikazi katika Idara hiyo.
Naibu Waziri, Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary
Mwanjelwa (Mb) akisoma kitabu cha Tanzania News Review kinachoonyesha
kuwa Mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere katika Maporomoko
ya Mto Rufiji unaojulikana
kama Julius
Nyerere HydroPower Project uliasisiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius
K. Nyerere mnamo mwaka 1975.
Naibu Waziri, Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary
Mwanjelwa (Mb) akishuhudia baadhi ya nyaraka muhimu zinazotunzwa na Idara ya
Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa wakati wa ziara yake ya kikazi katika Idara hiyo
jijini Dar es Salaam.
No comments :
Post a Comment