
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika, Bi. Anne Kabagambe (aliyeshika mkoba) akilakiwa na Mmoja waMaafisa wa TASAF, Bi. Tatu Mwaruka wakati wa ziara ya kukutana na Walengwa wa TASAF katika Mtaa wa Keko Machungwa wilaya ya Temeke Jijini Dar es salaam.

Bi. Anne Kabagambe (picha ya juu na chini) akiwa katika mkutano na walengwa wa TASAF katika mtaa wa Keko Machungwa ,wilaya ya Temeke, jijini Dar es salaam.


Baadhi ya Walengwa wa TASAF wakiwa na bidhaa walizozitengeneza baada ya kupata ruzuku kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini-PSSN.


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Bi. Anne Kabagambe akikagua bidhaa zilizotengenezwa na Walengwa wa TASAF mtaa wa Keko Machungwa,Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DuniaBi. Anne Kabagambe katika picha na Walengwa wa TASAF baada ya kukagua bidhaa wanazozitengeneza kama njia mojawapo ya kujiongezea kipato kkupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.
Na Estom Sanga -TASAF
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika, Bi.Anne Kabagambe
amepongeza mafanikio ya Serikali ya Tanzania Kupitia Mfuko wa Maendeleo
ya Jamii-TASAF katika kuboresha maisha ya Wananchi wanaokabiliwa na
Umaskini.
Bi.
Kabagambe ambaye yuko nchini kwa ziara ya Kikazi , ametoa pongezi hizo
baada ya kukutana na Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini
unaotekelezwa na TASAF,na kujionea bidhaa wanazozalisha katika Mtaa wa
Keko Machungwa ,Wilaya Temeke, mkoani Dar es salaam.
Amesema
kutokana na ubora wa Utekelezaji wa Miradi ya TASAF, Benki ya Dunia
imekubaliana na Serikali ya Tanzania kuidhinisha kiasi cha Shilingi
Trilioni Moja kwa ajili ya Utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya
Maskini Sehemu ya Pili , fedha ambazo amesema zitasaidia zaidi juhudi za
Serikali katika kuwahudumia Wananchi wanaokabiliwa na Umaskini.
‘’Tumejiridhisha
pasi na mashaka kuwa utekelezaji wa Shughuli za TASAF katika awamu zote
tatu umekuwa wa mafanikio makubwa hivyo Benki ya Dunia imeamua
kuendelea kusaidia juhudi hizi’’ amesisitiza Bi.Kabagambe.
Mkurugenzi
Mtendaji huyo wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika amesema kiasi hicho cha
fedha kitatolewa mwezi Ujao wa Septemba na kuwataka Walengwa na
Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kuendelea kuboresha miradi
ya kiuchumi ili kuongeza tija na hatimaye waweze kuboresha zaidi maisha
na kuondokana na umaskini wa kipato.
Kwa
Upande wao Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wameishukuru
Serikali kupitia TASAF kwa jitihada za kuwaondolea kero ya umaskini wa
kipato na kuomba juhudi zaidi zielekezwe katika kuwapatia elimu ya
Ujasiliamali ili waweze kuboresha shughuli za uzalishaji mali na kukuza
kipato chao.
Mfuko
wa Maendeleo ya Jamii – TASAF umekuwa ukitekeleza Mpango wa Kunusuru
Kaya Maskini ambao unahudumia takribani Kaya Milioni Moja na Laki Moja
Kote Tanzania Bara,Unguja na Pemba na hivi sasa uko katika maandalizi ya
utekelezaji wa Sehemu ya Pili ya Mpango inayotarajiwa kuzinduliwa hivi
karibuni baada ya taratibu muhimu kukamilika.
No comments :
Post a Comment