Mhe. Mtaka akisaini kitabu cha wageni kwenye banda la WCF |
Mkuu
wa Mkoa Mhe. Mtaka, akiongozana na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa WCF,
Bw. Sebera Fulgence baada ya kutembelea banda la Mfuko huo.
Mkurugenzi
wa Uendeshaji Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Anselim
Peter, (kulia), akitoa maelezo kuhusu shughuli za Mfuko kwa mwananchi
huyu aliyetembelea banda la WCF.
Afisa
Matekelezo Mwandamizi (WCF), Bw. Musa Mwambujule (kushoto),
akimuhudumia mwananchi huyu aliyetembelea banda namba 13 la WCF kwenye
viwanja vya Nanenane Nyakabindi Simiyu leo Agosti 1, 2019.
Mkurugenzi wa Uendeshaji Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Anselim Peter.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa WCF, Bw. Sebera Fulgence (kulia), akitoa elimu kwa mwananchi huyu aliyetembelea banda la Mfuko huo.
NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said, Simiyu
MKUU
wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka, ameupongeza Mfuko wa Fidia kwa
Wafanyakazi WCF, kutokana na ushiriki wake katika mpango wa Mkoa huo kuanzisha
kiwanda cha vifaa tiba kwa kutumia malighafi ya pamba.
Mhe.
Mtaka ametoa pongezi hizo kwenye viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu wakati
alipotembelea banda la WCF linaloshiriki maonesho ya Nanenane. mwaka 2019.
“Mimi
kama kiongozi wa serikali ya Mkoa, ninawashukuru sana WCF kama partner (washirika) wakubwa sana kwenye
mkoa wetu hususan kwenye ujenzi wa kiwanda cha vifaa tiba.” Alifafanua.
Alisema
WCF kupitia Mkurugenzi Mkuu wake, Bw. Masha Mshomba na wakurugenzi wengine
wamekuwa wakishirika wakubwa katika vikao vingi vya mkoa vinavyohitaji
washirika (partners).
Mkuu
huyo wa mkoa alisema, tayari site
clearance imefanyika na wizara inaelekea kutangaza zabuni ili mradi uanze
kutekelezwa.
Maonesho
ya Nanenane kitaifa yanayofanyika kwenye viwanja vya Nyakabindi nje kidogo ya
mji wa Bariadi yamefunguliwa rasmi leo Agosti 1, 2019 na Makamu wa Rais Mhe.
Samia Suluhu Hassan ambapo kaulimbiu ya mwaka huu inasema “Kilimo, Mifugo na
Uvuvi kwa ukuaji wa uchumi wa nchi.”
Akizungumzia
ushiriki wa WCF kwenye maonesho hayo, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko huo Bw.
Anselim Peter amesema, maonesho hayo ni fursa nzuri kwa Mfuko kuelimisha waajiri,
wafanyakazi na wananchi kwa ujumla kuhusu kazi na majukumu ya Mfuko.
“Tupo
hapa ili kutoa elimu kwa wafanyakazi, elimu kwa waajiri namna gani
wanaweza
kuwasilisha madai yao pale mfanyakazi anapopata madhara kutokana na kazi
ili hatimaye aweze kupata fidia stahiki na kwa wakati.” Alisema.
Amewakaribisha
wananchi wakiwemo waajiri kutoka Simiyu na mikoa jirani ya Shinyanga na Mara kufika
kwenye banda la WCF namba 13 lililo jirani na lango kuu la kuingia viwanja vya
Nyakabindi ili kupata elimu zaidi kuhusu huduma mbalimbali zitolewazo na WCF.
“Katika
banda letu, tunatoa huduma mbalimbali zikiwemo za waajiri kujisajili na Mfuko,
kwani tunatambua Mkoa wa Simiyu unakuja juu katika uwekezaji wa viwanda kwahivyo
tunategemea waajiri wapya wengi kutoka hapa.” Alisema.
No comments :
Post a Comment