Korea
kaskazini imefyatua kombora la masafa mafupi ambalo halijabainika mara
mbili , kwa mujibu wa maafisa wa Korea Kusini , katika jaribio la tatu
la silaha hizo katika kipindi cha wiki moja pekee.
Ufyatuaji wa makombora hayo ulifanyika katika eneo la mwambao wa mashariki mwa taifa hilo mapema Ijumaa.
Hatua
hiyo inaonekana kama hatua ya taifa hilo inayolenga kujibu mazoezi ya
kijeshi ya baina ya Korea Kusini na Marekani yanayotarajiwa kuanza mwezi
huu.
Wakati huo huo Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zimeitaka Korea kaskazini kushiriki mazungumzo ya "maana " na Marekani.
Baada
ya mkutano wa faragha katika baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ,
mataifa yalisema kuwa vikwazo vya kimataifa vinapaswa kuimarishwa hadi
utawala wa Pyongyang utakapoangamiza mipango yake ya nyuklia ya
makombora ya masafa.
Ufyatuaji
wa makombora hayo ulifanyika katika eneo la Yonghung katika jimbo la
South Hamgyong katika bahari ya Japan, inayofahamika pia kama Bahari ya
Masharik , kwamujibu wa Mkuu wa kikosi cha pamoja cha Korea kaskazini na
Korea Kusini (JCS).
Eneo
hilo linaonekana kama kituo cha kufyatulia makombora ambacho hakijawahi
kutumiwa awali , amesema Ankit Panda, afisa katika shirikisho la
wanasayansi wa Marekani - Federation of American Scientists.
"Hiki
ni kielelezo kingine cha enzi ya Kim Jong-un zaidi ya ufyatuaji wa
makombora ya usiku : kufyatua kutoka vituo ambavyo havikuwahi kutumiwa
awali au ambavyo havitumiwi"
No comments :
Post a Comment