Jaji
Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe Eliezer Feleshi(wa pili
kulia) akizungumza kuhusu mafanikio ya Mradi wa Maboresho ya Mahakama
ya Tanzania wa Miaka Mitano (2015/2016 mpaka 2019/2020) kwa ujumbe
kutoka Benki ya Dunia( wa kwanza kushoto) ni Mkuu wa Kitengo cha
Maboresho ya Mahakama ya Tanzania, Mhe. Zahra Maruma. (watatu kushoto)
Mtaalamu kutoka Benki ya Dunia, Benis Biseko (wanne kushoto) ni Msaidizi
wa Mtendaji wa Mkuu wa Tanzania,Ginaweda Nashon.Kulia wa kwanza
(kushoto) ni Mtaalamu kutoka Benki ya Dunia, Deborah Isser, wa pili
kushoto ni Mtaalamu kutoka Benki ya Dunia, Waleed Malik na watatu
(kushoto) ni Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Leonard Magacha.
Mkuu wa Kitengo cha Maboresho
ya Mahakama ya Tanzania (JDU)Mhe. Zahara Maruma (wa kwanza kushoto)
akijadiliana jambo na Wataalamu wa Benki ya Dunia, (wa pili) ni Deborah
Isser, (wa pili kushoto) ni Waleed Malik na wa kwanza ni Denis Biseko.
Mtaalamu kutoka Benki ya
Dunia,Deborah Isser(wa kwanza kulia ) akifafanua jambo kuhusu ueneshaji
wa kesi kwa njia ya mtandao ‘Video Conference’,(wa pili kulia) ni
Mtaalamu kutoka Benki ya Dunia, Waleed Malik na (watatu ni kulia) ni
Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Leonard Magacha.
***************
Na Aziza Muhali (SJMC)
30/08/2019
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya
Tanzania, Mhe. Dkt, Eliezer Feleshi, amefanya mazungumzo na wadau kutoka
Benki ya Dunia(WB) juu ya tathmini ya Mradi wa Maboresho ya Mahakama
ya Tanzania yanayofanywa chini, ambapo umeleta matokeo chanya katika
shughuli za Mahakama.
Akizungumza na ujumbe wa benki
hiyo, katika ofisi za Mahakama Kuu ya Tanzania, Jaji Kiongozi alisema
mradi huo, umeweza kusaidia kuboresha shughuli za utendaji kazi wa
Mahakama na kusogeza huduma karibu na wananchi.
“Tumeweza kusikiliza kesi kwa
kutumia Mahakama Inayotembea (Mobile Court) jijini Mwanza, hivyo ni moja
ya maboresho ya huduma za Mahakama, yaliyotokana na mradi huu,”
alisema Jaji Kiongozi.
Aliongeza kuwa mradi huo
unaofadhiliwa kwa fedha za mkopo kutoka benki hiyo, umewezesha
Mahakama ya Tanzania,kusikiliza kesi kwa njia ya Mtandao ‘Video
coference’, ambapo, ugeni huo, ulitaka kufahamu tathimini ya eneo hilo,
alisema umeweza kutumika katika baadhi ya mikoa,ambayo ni Mbeya,
Bukoba, na Kituo cha Mafunzo cha kilichopo katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu iliyo-Dar es Saalam, kikiwemo Chuo cha Uongozi wa
Mahakama(IJA) Lushoto.
Jaji Kiongozi amefafanua mkakati
wa kupata ukumbi(chumba maalum) kwa ajili ya kuanzisha kusikiliza kesi
kwa njia ya mtandao katika gereza la Keko Jijini Dar es Salaam.
Jaji kiongozi amefafanua
changamoto zinazoikabili Mahakama ikiwa ni pamoja na upungufu wa kumbi
maalumu za kuendeshea kesi kwa njia hiyo,‘Tunakabiliwa na upungufu wa
kumbi maalumu kwa ajili ya kuendeshea kesi, hivyo tunatakiwa tupate
kumbi nyingi ili tuweze kuendesha kesi kwa wakati.
Aliongeza kwamba kwa hivi sasa ni ukumbi mmoja ndio unaotumika kuendesha kesi kwa njia hiyo’, alisema Mh. Dkt. Jaji Kiongozi.
Aliyataja mafaniko mengine ni Mfumo wa Kusajili kesi kwa njia ya Kielektroniki(JSDS).
Dkt. Feleshi alisema eneo
lingine, ambalo litafanyikazi ni kuhusu ambayo upelelezi wa kesi
kuchukua muda mrefu ambapo kesi moja inaweza kuchukua kati ya mwaka
mmoja au zaidi, hivyo litawekewa muda maalum.
Wadau hao , waliwasili nchini
mnamo Agosti 23 mwaka huu , watakuwepo nchini hadi Agosti 31, mwaka
huu, wamefanya ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya ujenzi wa
Mahakama ikiwemo Mahakama ya Kuu ya Musoma, Mahakama ya Hakimu Mkazi
Simiyu na kufanya ziara Mkoani Dodoma na Mwanza ambako walijionea hali
halisi ya utendaji kazi wa Mahakama Inayotembea.
No comments :
Post a Comment