Wanachama na wadau mbalimbali wa Mfuko wa PSSSF waliokuwa
wametembelea banda la PSSSF kwenye maonesho ya 43 ya Biashara Kimataifa ya
Dar es Salaam, Sabasaba Julai mwaka huu, wakipewa huduma za aina mbalimbali na
wafanyakazi wa PSSSF.
Katika makala zilizopita ikumbukwe ya kuwa tuliona ya
kuwa katika mkakati wa kuboresha huduma na kupunguza matumizi katika sekta ya
hifadhi ya jamii nchini, Serikali iliamua kuunganisha Mifuko minne ya
PSPF, PPF, GEPF na LAPF na kuunda Mfuko mmoja unaojulikana kama...
Mfuko wa hifadhi ya jamii kwa watumishi wa umma (PSSSF).
Mfuko wa hifadhi ya jamii kwa watumishi wa umma (PSSSF).
Hivyo basi Serikali kupitia
sheria ya mfuko wa hifadhi ya jamii kwa watumishi wa umma namba 2 ya mwaka 2018
ilifuta mifuko ya hifadhi ya jamii ya PPF, PSPF, LAPF, na GEPF na kuanzisha
mfuko wa hifadhi ya jamii kwa watumishi wote wa umma yaani PSSSF.
Ambapo kuanzia Agosti Mosi,
2018, waliokuwa wanachama wa mifuko iliyounganishwa yaani PPF, PSPF, LAPF, na
GEPF waliohamishiwa katika mfuko wa PSSSF hivyo wataendelea kuwa wanachama na
kuchangia katika mfuko wa PSSSF. Wanachama wa mfuko wa PSSSF ni pamoja wataafu
na wategemezi wao waliokuwa wanalipwa pensheni na mifuko iliyounganishwa.
Na
majukumu makubwa ya mfuko huu wa PSSSF ni kuandikisha wanachama, kukusanya
michango, kuwekeza michango hiyo na kulipa mafao. Mafao yanayotolewa na mfuko
huu wa hifadhi ya jamii yamegawanyika katika makundi mawili, makundi hayo ni
mafao ya muda mrefu na mafao ya muda mfupi.
Mafao
ya muda mfupi ni; fao la uzazi, fao la ugonjwa, fao la kupoteza ajira, na
msaada wa mazishi. Mafao ya muda mrefu ni pensheni ya ulemavu, pensheni ya
urithi pamoja na pensheni ya uzee.
Wakati
huo huo mfuko unatoa msaada wa huduma ya elimu kwa watoto mpaka kumaliza elimu
ya juu kwa wale ambao mzazi wao walikuwa mwanachama wa PSSSF wakati wa uhai wao.
Sheria
ya mfuko wa hifadhi ya jamii PSSSF ya mwaka 2018
inatoa amana
ya mkopo wa nyumba ya makazi katika kutambua umuhimu wa jambo hili kwa wastaafu
wake.
Inatamka
wazi ya kuwa mwanachama wa mfuko wa PSSSF anaweza kutumia sehemu ya mafao yake
kama dhamana ya kupata mkopo wa nyumba ya makazi kulingana na utaratibu
ulioelekezwa na mamlaka. Na kuonesha ya kuwa sheria hiyo inakwenda na wakati
hasa kwa kuwajali wateja wake inasema wazi ya kuwa mwanachama anaweza kwa
ruhusa ya bodi kuchukua sehemu ya michango yake kwa namna na kwa kiasi
kitakachokuwa kimeainishwa kwenye Kanuni kulingana na kifungu cha 38 cha sheria
ya Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA)
Kulingana na sheria ya
PSSSF ya mwaka 2018 amana ya mwanachama”
maana yake ni michango ya mwajiriwa, michango ya mwajiri na riba yake ambayo
ipo kwenye akaunti ya mwanachama. Sheria hiyo
inaruhusu wanachama wake kuingilia michango yao ya akiba ya pensheni kwa ajili
ya amana ya kujipatia nyumba ya mkopo. Mkopo huu ni kwa ajili
ya kujenga nyumba ya mwanachama wa PSSSF na hutolewa kwa mwanachama
aliyefikisha umri wa miaka 55 ambaye amechangia kwa muda usiopungua miezi 180.
Mpaka kufikia sasa,
Mfuko wa PSSSF una jumla ya wastaafu wapatao 124,000 na wanachama 763,000 na
watumishi wa PSSSF wakiwa wamejipanga kutoa huduma bora kwa wastaafu na
wanachama wa mfuko huu wa PSSSF katika ofisi zote za Mfuko zilizo Tanzania bara
na Visiwani zilizofunguliwa tangu Mfuko
huu uanze shughuli zake Agosti Mosi, 2018.
Thamani
ya Mfuko wa pensheni kwa watumishi wa umma (PSSSF) mpaka sasa imefikia Sh.
trilioni 5.8 za Kitanzania. Hivyo kuunganishwa kwa mifuko ya GEPF, LAPF, PSPF
na PPF kunatoa fursa ya kuimarisha zaidi sekta ya hifadhi ya jamii hali
iliyochangia thamani ya mfuko mpya wa PSSSF kuendelea kukua hata katika kipindi
kifupi tangu kuanzishwa kwake.
Mfuko unahakikisha ya kuwa wastaafu
wote waliohakikiwa wanalipwa mara moja ili kutekeleza dhamira ya mfuko
inayohakikisha wanachama na wastaafu wake wanalipwa kwa wakati muafaka na
kwa uhakika.
Zaidi
ya elfu kumi ya wastaafu wameshalipwa mafao yao tangu kuanzishwa kwa mfuko huu
wa PSSSF mwaka 2018 na wachache ambao hawajalipwa ni wale ambao hawajahakiki
taarifa zao kwa muda uliotolewa hivyo wanatakiwa kujitokeza na kuhakikiwa ili
warejeshwe katika daftari la malipo.
Baadhi
ya mafao yanayoendelea kutolewa na PSSSF ni yale ya muda mfupi na muda mrefu
lengo likiwa kuwawezesha wanachama wote kuishi maisha bora hata baada ya
kustaafu.
PSSSF
inaendelea kutoa elimu ya hifadhi ya jamii na semina ya maandalizi ya kustaafu
kwa wanachama wake mahali pa kazi.
Mfuko
wa PSSSF hutoa huduma ya uzazi na msaada wa mazishi bure. Kufaidika na mafao
ya mazishi na uzazi hakuathiri hata kidogo michango ya mwanachama.
Wanachama
wa PSSSF wataendelea kunufaika na huduma za PSSSF na hata pale inapotokea
bahati mbaya mwanachama wake amefariki basi haki zake hazitapotea na zinalindwa
kwa mujibu wa sheria ili ziwanufaishe warithi wake.
Mfuko
wa PSSSF umejenga mifumo bora ya teknolojia ya habari na mawasiliano
inayounganisha ofisi zote na makao makuu ya mfuko ili kuimarisha huduma na tija
kwa wanachama.
Wanachama wa PSSSF wanayo fursa ya kupata
taarifa za michango yao katika ofisi zote za PSSSF nchi nzima pamoja na kupitia
simu za mkononi.
Wanachama wanaweza kuwasiliana na Mfuko ili
kupata ufafanuzi wa masuala yao, maswali au malalamiko kwa kupiga simu kupitia
namba 0800 110 055, 0800 780 060 na 0800 110 040, namba hizi ni bure. Pia
wanaweza kutuma ujumbe mfupi kwa namba 0735 117 773 na 0736 117 773
Wanachama wa PSSSF wanaweza kufungua madai yao
katika katika ofisi yeyote ya PSSSF iliyoko karibu nao, zilizosambaa karibu
mikoa yote 29 na wilaya zote za Tanzania bara na Zanzibar visiwani ili kuongeza
ufanisi na kusogeza huduma karibu na wanachama na wadau wake.
Mfuko
wa PSSSF ni matokeo ya kuunganishwa kwa mifuko ya PSPF, LAPF, GEPF na PPF ili
kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi na hasa kuchochea ukuaji wa sekta ya
hifadhi ya jamii hapa nchini.
Mpaka sasa Mfuko umeshatumia zaidi
ya trilioni moja kulipa mafao kwa wanachama wake hali inayoonesha kuwa mfuko
upo katika hali nzuri kiafya, hivyo mfuko wa PSSSF umejipanga ya kuwa
unahakikisha unawahudumia wanachama na wadau wake vizuri kwa mujibu wa sheria
na kanuni za hifadhi ya jamii.
No comments :
Post a Comment