Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) anayeshughurikia afya Dk. Doroth Gwajima,akizungumza na
watumishi wa kituo cha afya cha Chamwino Ikulu alipofanya ziara ya
kukagua utoaji huduma za afya kwa wateja wenye kadi za CHF
iliyoboreshwa.

Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) anayeshughurikia Afya Dk.Doroth Gwajima,akiwaonyesha kadi ya
CHF iliyoboreshwa wananchi waliofika katika kituo cha Afya cha Chamwino
Ikulu alipofanya ziara ya kukagua utoaji huduma za afya kwa wateja wenye
kadi za CHF iliyoboreshwa huku akiwahimiza zaidi ili wajiunge na wapate
huduma iliyobora.

Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) anayeshughurikia Afya Dk.Doroth Gwajima,akizungumza na baadhi
ya wananchi waliofika katika kituo cha Afya cha Chamwino Ikulu
alipofanya ziara ya kukagua utoaji huduma za afya kwa wateja wenye kadi
za CHF iliyoboreshwa huku akiwahimiza zaidi ili wajiunge na wapate
huduma iliyobora.
Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) anayeshughurikia afya Dk. Doroth Gwajima, amewataka watumishi
wa afya kote nchini kuacha kuwabagua au kutowapa kipaumbele wateja
wanaotumia kadi za bima ya afya ya jamii CHF iliyoboreshwa kwa
kuwahudumia watu wenye fedha mkononi kwanza.
Dk.
Gwajima ameyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na watumishi wa
kituo cha afya cha Chamwino Ikulu alipofanya ziara ya kukagua utoaji
huduma za afya kwa wateja wenye kadi za CHF iliyoboreshwa wilayani hapo.
Amewataka
watumishi wa afya kuwapa kipaumbele wagonjwa wanaotumia kadi hizo ili
kuweza kuongeza idadi ya watu wanaotumia mfumo huo nchini.Dk Gwajima
Amewataka watumishi kote nchini kuendelea kuhamasisha matumizi ya kadi
hizo ili kuongeza idadi ya watu wanaotumia mfumo huo hapa nchini na watu
wengi waweze kujiunga.Amesema hivi sasa kadi za CHF iliyoboreshwa
imefanyiwa marekebisho makubwa na serikali hali ambayo inamwezesha
mgonjwa kupata huduma katika hospitali yoyote hadi ngazi ya mkoa.
Pia
amewataka watumishi wa afya nchini kutoa huduma zenye ubora ili kuweza
kuwavutia wananchi kujiunga na mifumo hiyo ya bima ya afya ya
jamii.“Kama tusipotoa huduma bora hivi vituo vyetu tulivyojenga nchi
nzima vitakuwa havina maana lazima sisi kama watumishi wa afya
tubadilike ili kuweza kuwavutia wananchi kuja katika vituo vyetu kupata
huduma ya afya”
“Sitaki
kusikia baada ya siku hizi 14 kuwa kuna kituo kimeshindwa kutuma
taarifa zake au mifumo inakataa kwani kila kituo kinatakiwa kutuma
taarifa zake za wateja waliohudumiwa ili kuweza kurejeshewa fedha zake
ambazo zitatumika katika mahitaji mbalimbali ya eneo hilo”amesema Dkt
Gwajima.
Naye
mganga mfawidhi wa kituo cha afya Chamwino, Dk. Zipora Mfugale amesema
kuwa wamejipa kuhakikisha kuwa wanaongeza idadi ya watu wanaotumia mfumo
wa CHF iliyoboreshwa.

No comments :
Post a Comment