Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa, (wapili kushoto), akimpongeza Bw. Siyovelwa kwa tuzo hiyo.
Balozi Seif Ali Iddi akihutubia katika hafla hiyo.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa, akitoa hotuba yake.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano WCF, Bi. Laura Kunenge (mwenye nguo nyeupe), akifuatilia utoaji wa tuzo hizo
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Abraham Siyovelwa (mwenye tai nyekundu),
akiwa kwenye hafla hiyo kabla ya kuitwa kupokea tuzo hiyo.
Bw. Siyovelwa akiwa na timu iliyokuwa ikitoa huduma kwenye banda la WCF ,mara baada ya kupokea tuzo hiyo.
Afisa Uhusiano WCF, Bi. Sarah (kushoto), akimpatia maelezo mwananchi huyu aliyetembelea banda la WCF Julai 11, 2019.
MFUKO
wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umetwaa tuzo ya mshindi wa pili kundi la Sekta
ya Hifadhi ya Jamii pamoja na Sekta ya Bima kwa kuwa banda lililotoa huduma
bora kwenye maonesho ya 43 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam 2019
katika kundi hilo.
Makamu
wa Pili wa Rais, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi ndiye aliyemkabidhi tuzo hiyo, Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Abraham Siyovelwa wakati wa hafla ya ufungaji rasmi
wa maonesho hayo kwenye ukumbi wa Rashid Mfaume Kawawa (Ceremonial dome), uwanja wa Maonesho wa Mwalimu J.K Nyerere, maarufu
Sabasaba, barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam Julai 11, 2019.
Ufungaji
huo ni sehemu tu ya taratibu lakini maonesho yataendelea hadi Julai 13, 2019,
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uendelezaji Biashara (TanTrade),ambao ndio
waandaaji wa maonesho hayo, Bw. Edwin Mutageruka alisema.
Akizungumzia
ushidi huo Bw. Siyovelwa alisema, “Tunafuraha
kubwa kama Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, huu ni mwaka wa pili tunapata tuzo na
mwaka huu tumepanda zaidi mwaka jana tulishinda kwenye Sekta ya Hifadhi ya
Jamii lakini mwaka huu tumekuwa washindi wa pili kwenye Sekta ya Hifadhi ya
Jamii pamoja na Bima.” Alifafanua Bw. Siyovelwa ambaye pia ni Mkuu wa
Sheria wa Mfuko huo.
Akizungumzia
huduma walizokuwa wakitoa kwenye banda la WCF katika maonesho hayo
yaliyoshirikisha mataifa zaidi ya 35 kutoka sehemu mbalimbali duniani, Bw.
Siyovelwa alifafanua “Pamoja na kutoa huduma nyingine zote lakini tuliona lengo
letu liwe kutoa elimu zaidi kwa wafanyakazi na waajiri ya namna ya kudai fidia
pale wanapopatwa na matatizo kwa sababu tumeona ni changamoto kubwa ambayo
inatukabili.” Alisema.
No comments :
Post a Comment