Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale, Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo, (kulia), akiwa amebeba pakiti
ya korosho huku akipatiwa maelezo na Afisa Masoko Bodi ya Nafaka na Mazao
Mchanganyiko, Bw. Peter Mobe ya namna ya kuandaa korosjo hizo tayari kwa mauzo toka
kwa wakati alipotembelea banda la Bodi ya Nafaka na Mazao Machanganyiko kwenye
maonesho ya 43 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, viwanja vya Sabasaba
jijini Dar es Salaam, Julai 11, 2019.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
Waziri
wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe.
Mahmoud Thabit Kombo, amefurahishwa na kazi zinazofanywa na Bodi ya Nafaka na
Mazao Mchanganyiko Tanzania (CPB) hususan namna ya ufungashaji wa korosho.
Mhe.
Kombo ametembelea banda hilo leo Julai 11, 2019 ambapo alipata maelezo ya
shughuli za bodi hiyo kutoka kwa Afisa Masoko, Bw. Peter Mobe ambaye alisema
Bodi inafanya kazi ya kungeza thamani ya mazao kabla ya kuyapeleka sokoni.
“Tunanunua
mazao kutoka kwa wakulima, na kisha tunaongeza thamani ya mazao hayo kabla ya
kupeleka kwenye soko ndani na nje ya nchi” Alisema Bw. Mobe.
Alisema
Bodi ya Nafaka na Mazao Machanganyiko ni Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa mwaka 2009 kwa Sheria namba 19
ikiwa na lengo la kufanya biashara ya Mazao ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko.
“Kwa
sasa tunazo bidhaa za Unga wa dona unaitwa Dona Bora au chama nguvu, pia tuna
Korosho ambayo tumeipa jina Korosho ya Tanzania au TanKorosho.” Alibainisha Bw.
Mobe.
Naye
Waziri Kombo alisema amefurahishwa na namna bidhaa hizo zinavyofungashwa hususan
korosho kwani ufungashaji huo unawezesha bidhaa kukaa kwa muda mrefu bila
kuharibika na hivyo kuna umuhimu wa taasisi zinazoshughulika na ufungashaji
mazao huko Zanzibar zikafanya ushirikiano wa kubadilishana ujuzi na uzoefu na
Bodi hiyo ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko Tanzania.
No comments :
Post a Comment