Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, akibonyeza kitufe, wakati akizindua
zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, katika viwanja vya Mandela
mkoani Kilimanjaro Julai 18.2019. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu).
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Walemavu,
Jenista Mhagama, katika uzinduzi wa daftari la kudumu la wapiga kura,
uliyofanyika kwenye viwanja vya Mandela mkoani Kilimanjaro Julai 18.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, akiketa jambo na Mwenyekiti wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi, Jaji Semistocles Kaijage, kabla ya uzinduzi wa
daftari la kudumu la wapiga kura, uliyofanyika kwenye viwanja vya Mandela
mkoani Kilimanjaro Julai 18.2019. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu).
Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Walemavu,
Jenista Mhagama, akizungumza na wananchi waliyohudhuria
katika uzinduzi wa daftari la kudumu la wapiga kura, uliyofanyika kwenye viwanja
vya Mandela mkoani Kilimanjaro Julai 18.2019. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwahutubia wananchi
waliyohudhuria katika uzinduzi wa daftari la kudumu la wapiga kura,
uliyofanyika kwenye viwanja vya Mandela mkoani Kilimanjaro Julai 18.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwahutubia wananchi
waliyohudhuria katika uzinduzi wa daftari la kudumu la wapiga kura,
uliyofanyika kwenye viwanja vya Mandela mkoani Kilimanjaro Julai 18.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, akishuhudia kijana Nehemia Mhando, akiandikishwa
kwenye daftari la kudumu la wapiga kura, katika uzinduzi wa daftari hilo,
uliyofanyika kwenye viwanja vya Mandela mkoani Kilimanjaro Julai 18.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, akimkabidhi kadi ya kupigia kura, kijana
Nehemia Mhando, baada ya kuzindua daftari la kudumu la wapiga kura,
katika uzinduzi wa daftari hilo, uliyofanyika kwenye viwanja vya Mandela mkoani
Kilimanjaro Julai 18.2019. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu). *Ahimiza vijana wajitokeze kwa wingi, aonya asasi za kiraia za kutoa elimu ya mpigakura zisijihusishe na ushabiki wa kisiasa
NA OWM, ARUSHA
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua rasmi zoezi la uboreshaji wa
Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na kuwahimiza vijana waliotimiza miaka 18 wajitokeze
kwa wingi kujiandikisha.
“Nitoe rai kwa
vijana wote wa Kitanzania waliotimiza umri wa miaka 18 au wale ambao watatimiza
umri huo ifikapo Oktoba, 2020 wajitokeze kwa wingi na kujiandikisha katika
Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Hawa ndio walengwa wakuu kwa sababu wanaingia
kwa mara ya kwanza katika uchaguzi.”
“Ikumbukwe
kwamba, bila kujiandikisha hawataweza kutumia haki yao ya msingi ya kuchagua
viongozi wanaowataka. Hivyo, kujiandikisha kwao kutawahakikishia ushiriki wao katika
uchaguzi wa viongozi,” amesema Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu ametoa rai hiyo leo, (Alhamisi, Julai 18, 2019) wakati akizindua
zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura lililofanyika kwenye
uwanja wa Mandela, Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Waziri Mkuu ambaye amewasili mkoani Kilimanjaro leo asubuhi kwa ziara ya
kikazi za siku nne, ametumia fursa hiyo kuwasisitiza vijana na wale wanaorekebisha
taarifa zao kwamba hakuna mtu atakayeruhusiwa kupiga kura katika uchaguzi mkuu
wa mwaka 2020 kama hajajiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ama
hana kadi ya mpigakura.
Amesema zoezi hilo ambalo limeanza leo, linafanyika kwa mara ya kwanza
tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Amesema litafanyika nchi
nzima na linatarajiwa kukamilika Machi, 2020.
“Watakaohusika awamu hii ni wapigakura waliotimiza miaka
18 hivi karibuni, wale watakaotimiza miaka 18 wakati wa Uchaguzi Mkuu Oktoba 2020,
waliohama kata au Jimbo na kuhamia maeneo mengine ya kiuchaguzi, waliopoteza
kadi au kadi zao kuharibika, wanaohitaji kurekebisha taarifa zao mfano majina
ambayo hapo awali yalikuwa yamekosewa sambamba na kuwaondoa wapiga kura waliopoteza
sifa kama vile kufariki,” amesema.
Katika hatua
nyingine, Waziri Mkuu ameziasa asasi
za kiraia ambazo zimepewa vibali vya kutoa elimu ya mpigakura, zijiepushe na
ushabiki wa kisiasa na badala yake zizingatie mwongozo wa elimu ya mpigakura uliotolewa
na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
“Nimeambiwa, Tume imetoa vibali vya kutoa elimu ya mpigakura kwa baadhi
ya Asasi za Kiraia. Rai yangu kwa asasi zilizopata vibali hivyo ni kuendelea
kutoa elimu hiyo kwa wananchi kwa kuzingatia mwongozo wa uliotolewa na Tume ya Taifa
ya Uchaguzi. Niendelee kuwaasa pia kutohusisha ushabiki na mijadala ya kisiasa
muda wote mtakapokuwa mkitoa elimu hiyo,” amesema.
Amesema ana imani kuwa wananchi wakipata elimu kuhusu uboreshaji kama
inavyoendelea kutolewa, basi watahamasika kutumia haki yao ya kikatiba ya
kujiandikisha katika daftari hilo na hatimaye kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa
mwaka 2020.
Amesema zoezi la majaribio ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga
Kura katika Kata ya Kibuta katika Halmshauri ya Wilaya ya Kisarawe na Kata ya
Kihonda katika Halmashauri ya Manispaa ya Wilaya ya Morogoro, lilifanyika kwa
mafanikio makubwa.
Mapema, akitoa maelezo kuhusu zoezi hilo, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Semistocles Kaijage, alisema katika zoezi la
sasa, Tume itaendelea kutumia teknolojia ya kielektroniki ya Biometric (BVR) na imeandaa BVR kits 3,000.
Alisema kwa
Tanzania Bara, Tume hiyo imeongeza vituo vya uandikishaji kutoka
36,549 vilivyotumika mwaka 2015 hadi kufikia 37,407; kutokana na zoezi la uhakiki wa vituo vya kuandikisha wapiga kura lililoendeshwa mwaka
jana.
“Kutokana na hilo, vituo 6,208 vilibadilishwa
majina, vituo 817 vimehamishwa kutoka mtaa mmoja au kijiji kimoja na kwenda
kingine na vituo 19 vilihamishwa kutoka kata moja kwenda kata nyingine.”
“Kwa upande wa Zanzibar, vituo vya uandikishaji
vimeongezeka kutoka 380 na kufikia 407. Kwa sasa kila kijiji au mtaa, utakuwa
na kituo kimoja,” alisema.
Alisema vituo vya uandikishaji vitafunguliwa saa 2
asubuhi hadi saa 12 jioni na zoezi la uboreshaji litafanyika kwa siku saba kwa
kila kituo cha kujiandikisha iwe ni Tanzania Bara au Zanzibar.
No comments :
Post a Comment