RAIS
wa Kenya, Uhuru Kenyatta amemtumia ujumbe maalumu Rais wa Tanzania,
Dkt. John Magufuli unaoelezea msimamo wa Serikali yake kuhusu kukerwa na
matamshi yaliyotolewa hivi karibuni na Mbunge wa jimbo la Starehe,
Charles Njagua Kanyi maarufu kwa jina la Jaguar.
Akipokea taarifa hiyo Waziri Mkuu amesema Watanzania wamefurahishwa na
hatua mbalimbali zilizochukulia na Serikali ya Kenya dhidi ya mbunge
huyo zinazodhihirisha kwamba matamshi hayo hayakuwa msimamo wa Serikali
ya Kenya wala wananchi wake bali ulikuwa ni msimamo binafsi wa mbunge
huyo.
Amesema siku zote Watanzania na Wakenya wamekuwa huru kuishi na kufanya
kazi au biashara katika nchi za Afrika ya Mashariki na pale yalipotokea
matatizo au kutokukubaliana serikali husika zilikaa mezani na kumaliza
tofauti hizo.
"Uhusiano kati ya Kenya na Tanzania ni wa karibu mno na wa kidugu kwani
kuna baadhi ya makabila yapo katika nchi mbili hizi kama vile Wamasai na
Wakurya na Wajaluo hivyo ushirkiano katika masuala ya mbalimbali
yakiwemo ya kabiashara na ya kijamii haukwepeki."
Hivyo, Waziri Mkuu ametoa wito kwa viongozi na wananchi wa nchi za
Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kujiepusha na kauli zenye viashiria vya
kujenga chuki, uhasama na migongano miongoni mwa wananchi kwani kauli
hizo zisipodhibitiwa mapema zinaweza kusabisha hofu na kutokuelewana
miongoni mwao.
Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwasihi Watanzania kuendelea kuishi
kwa amani na upendo na ndugu zao wa Kenya na wageni wote kutoka nchi za
Afrika ya Mashariki na duniani kwa ujumla ambao wapo nchini wakifanya
shughuli mbalimbali kwa mujibu wa sheria za nchi.
“Mambo yetu yote katika nchi za Afrika ya Mashariki hasa ya biashara na
ya kiuchumi kwa ujumla yataenda vizuri endapo tutalinda na kudumisha
amani, bila amani tutaogopana na tutashindwa kabisa kushirikiana”,
amesisitiza Mheshimiwa Majaliwa.
Waziri Mkuu ameahidi kuwa Serikali ya Tanzania kamwe ahaitaruhusu wala
kufumbia macho kauli au vitendo vyovyote vyenye viashiria vya uchochezi
dhidi ya nchi jirani ili na kulinda na kuunga mkono juhudi mbalimbali
za ushirikiano wa kisiasa na kiuchumi zinazofanywa na viongozi wakuu wa
Mataifa ya Afrika.
Kwa upande wake Balozi Kazungu amemshukuru Waziri Mkuu kwa kauli yake
aliyoitoa Bungeni jijini Dodoma iliyowataka Watanzania kuwa watulivu na
wayachukulie matamshi ya Mbunge wa jimbo la Starehe nchini Kenya, Njagua
kuwa ni msimamo wake binafsi na siyo msimamo wa Wakenya na Serikali
yao.
Balozi Njagua mesema Msimamo wa Rais Kenyatta siku zote umekuwa ni
kuwapokea na kuwakubali ndugu zao wote wanaotoka nchi za Jumuiya ya
Afrika Mashariki walioamua kuishi au kufanya biashara nchini Kenya.
Mwanzoni mwa wiki iliyopita Mbunge wa jimbo la Starehe nchini Kenya
Njagua alitoa matamshi ya kichochezi akiwataka raia wa kigeni kutoka
Mataifa mbalimbali wanaofanya shughuli za kibiashara nchini Kenya
wakiwemo Watanzania waondoke ndani ya muda wa saa 24.
No comments :
Post a Comment