
“Huu
ni utamaduni mpya ambao haukubaliki na ningependa kuchukua nafasi hii
kusema kwamba suala la utekaji na watu kupotea linaweza kuiondolea nchi
yetu heshima duniani tangu tupate uhuru, hivyo ningependa kuwaomba
viongozi wote walikemee,”
“Viongozi wa serikali wasione aibu hata wa Dini wasiogope na wastaafu
wote lazima tukemee utamaduni huu mpya, hatuwezi kuendelea kuishi katika
nchi yenye watu wenye wasiwasi na uoga ambao hawajui kesho wataamka
vipi na hii ajenda iishe maana isipo isha itaenda kwenye uchaguzi
mwakani,” Membe
Aidha, akizungumzia kuhusu Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu
kupoteza ubunge, Membe amesema kama Mtanzania ameshangaa sana.
“Mimi kama Mtanzania nilishangazwa sana na uamuzi wa Spika, Job Ndugai lakini tusubiri Lissu arudi.
“Nina uhakika atakwenda mahakamani kudai haki yake na kama ipo haki ataipata mahakamani,” amesema Membe
No comments :
Post a Comment