Mtendaji
Mkuu Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale
akisaini Mkataba wa ujenzi wa Daraja la Kigongo-Busisi mkoani Mwanza na
Mwakilishi kutoka kampuni ya ujenzi ya China Civil Engeering
Construction Coorporation, Zhang Jang, katika hafla iliyofanyika Makao
makuu ya Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA, Jijini Dar es Salaam,
wanaoshuhudia ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi
Isack Kamwelwe na Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jaffo.
Mtendaji
Mkuu Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale
na Mwakilishi kutoka kampuni ya ujenzi ya China Civil Engeering
Construction Coorporation, Zhang Jang, wakionesha nakala za mkataba wa
ujenzi wa Daraja la Kigongo- Busisi mara baada ya kusainiwa, ujenzi wake
utagharimu TZS. Bilioni 592. (Picha Idara ya Habari-MAELEZO).
Hatimaye
historia imeandikwa nchini Tanzania kwa kusainiwa kwa mkataba wa ujenzi
wa daraja la Kigongo Busisi katika Ziwa Victoria mkoani Mwanza lenye
urefu wa kilometa 3.2, ambao utagharimu jumla ya fedha za kitanzania
Bilioni 592.
Akizungumza
Jijini Dar es Salaam katika hafla ya utiaji saini mkataba wa ujenzi wa
daraja hilo, Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaac
Kamwelwe, amesema mradi huo utatekelezwa kwa fedha za walipa kodi wa
Tanzania bila kutegemea fedha za wafadhili.
Waziri
Kamwelwe alisema mradi wa Kigongo Busisi kama ilivyo miradi mingine ya
kimkakati ulipigwa vita sana na baadhi ya watanzania na hata wahisani,
amesema hata
No comments :
Post a Comment