Monday, July 29, 2019

KAMPENI YA NSSF NA MARAFIKI YALETA MATOKEO CHANYA


Picha inayohusiana

SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limeendelea kuandikisha wanachama wapya kutoka kwenye sekta binafsi na sekta isiyokuwa rasmi kupitia kampeni ya NSSF na MARAFIKI iliyoanzishwa mwishoni mwa wiki iliyopita.

Kupitia kampeni hiyo NSSF inapita kwa kila mwajiri ili kuhakikisha wanasajili wafanyakazi wao na kuwakilisha michango ya wafanyakazi wao kwa wakati.
SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) hivyo limeandikisha  wanachama wapya 472 kwenye sekta binafsi na sekta isiyo rasmi kupitia kampeni ya ‘NSSF na MARAFIKI’ iliyoanzishwa mwishoni mwa wiki iliyopita.
Meneja Kiongozi Uendeshaji wa NSSF, Cosmas Sasi, anasema haya baada ya  kutembelea kampuni ya...
KK Security Mkoa wa Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Anasema kupitia kampeni hiyo, NSSF itapita kwa kila mwajiri ili kuhakikisha wanasajili wafanyakazi wao na kuwasilisha michango ya wafanyakazi wao kwa wakati.
"Tumezindua kampeni maalumu inayoitwa ‘NSSF na MARAFIKI’.  Kupitia kampeni hii, tunapita kwa waajiri wote Tanzania nzima kuhakikisha waajiriwa wote wanaandikishwa. Kampeni hii ni ya kirafiki ambayo waajiri sasa wanashirikiana na NSSF kuhakikisha wafanyakazi  wao wanaandikishwa kwenye mfuko ikiwa ni takwa la kisheria," anasema Sasi.
Meneja wa NSSF Mkoa wa Kinondoni, Hiza Kiluwasha, anasema dhana ya kampeni hiyo  ni kuwapatia elimu wanachama kuhusu umuhimu wa kujiunga na  kuchangia NSSF.
"Kampeni yetu mpya kabisa sasa hivi ni NSSF na MARAFIKI kwa hiyo marafiki wetu   ni wanachama wa NSSF na waajiri, sasa kuhakikisha rafiki yako lazima uwe unamtembelea kila wakati pia kwa marafiki zetu wote ambao bado hatujawafikia kwa kuzingatia kampeni hii basi waje katika ofisi zetu za NSSF kwa ajili ya kujiandikisha au kupiga simu " anasema.
Naye Mwakilishi wa Idara ya Rasilimali Watu wa KK Security, Victor Gaudence, anaishukuru NSSF kwa kuwatembelea na kutoa elimu ya hifadhi ya jamii iliyofanikisha kusajili wafanyakazi 472 wa kampuni hiyo.
Kutokana na mabadiliko ya Sheria ya Hifadhi ya Jamii ya mwaka 2018, NSSF inatoa huduma ya hifadhi ya jamii kwa sekta binafsi na sekta isiyo rasmi, hivyo kampeni hiyo itasaidia kuongeza wanachama kutoka katika sekta hizo.

No comments :

Post a Comment