Baada
ya uzinduzi wa hifadhi hiyo Jumanne Julai 9, 2019 uliofanywa na Rais
John Magufuli, mjadala uliibuka katika mitandao mbalimbali ya kijamii
kuwa sanamu haifanani na mwonekano wa Rais wa Awamu ya Kwanza.
Lakini Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla amesema kama
kuna upungufu wizara hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo ndiyo wenye dhamana ya kuangalia kama ina
kasoro ili ifanyiwe marekebisho.
Waziri huyo amesema wana wataalam watakaoitazama sanamu hiyo na kujua kama ina upungufu na kurekebishwa.
"Kwa
nia njema kabisa Wizara yetu iliamua kumpa tuzo maalum Rais Magufuli
ambayo ina maneno aliyoyasema Mwl. Nyerere mwaka 1961, lakini nimeona
imezua mjadala sana kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii
jambo ambalo ni zuri imeweka alama
“Hatuyapuuzi
maneno na comment za Watanzania wenzetu ambayo yanahusiana na uumbaji
wa lile sanamu,kama kuna mapungufu sisi ndio wenye dhamana ya kuangalia
kama liko sahihi, Wataalamu tunao Serikalini tutawaita watuelekeze kama
kuna mapungufu yatarekebishwa
“Vijana
na Wanasiasa wanaozungumza kwenye mitandao tunawashukuru kwa comment
zao na tunawatoa wasiwasi kuwa tutalishughulikia, jambo ambalo
limenifurahisha ni kwamba vijana bado wanaikumbuka taswira halisi ya
Mwl.Nyerere,ni jambo kubwa sana kwetu kama Taifa.”
“Nimefurahishwa
pia na mjadala wa faru Rajabu ambaye pia yupo kwenye mikono salama ya
TANAPA na anaendelea kufanya kazi yake vizuri kabisa bila shida,
tutatafuta mtoto wake mmoja machachari tutamleta kwenye Hifadhi ya
Burigi Chato" Amesema Kigwangalla.
==>>Msikilize hapo chini
No comments :
Post a Comment