Boti
tano zenye silaha zinazoaminika kuwa za Jeshi la Iran zimejaribu leo
kuimakamata meli ya mafuta ya Uingereza katika eneo la Ghuba bila
mafanikio, Shirika la Utangazaji la CNN limeripoti likiwanukuu maafisa
wawili wa Marekani wakisema, kuwa meli hiyo ya Uingereza ilikuwa
ikiingia katika mlango bahari wa Hormuz wakati boti tano zilipoikaribia
na kuiamuru kusimama katika mipaka ya bahari ya Iran.
Hata
hivyo meli ya kivita ya Uingereza iliyokuwa ikiisindikiza meli hiyo ya
mafuta ilitishia kuzishambulia boti za Iran na kuziamuru kuondoka.
Kisa
hicho kinajiri siku chache tangu Uingereza ilipoikamata meli ya mafuta
ya Iran katika eneo la Gibraltar kwa madai ya kukiuka vikwazo vya Umoja
wa Ulaya dhidi ya Syria.
Tukio
hilo lilizusha mzozo mkubwa wa kidiplomasia kati ya Iran na Uingereza
na Tehran ilitishia kuwa itakamata meli ya mafuta ya Uingereza kama
hatua ya kulipa kisasi.
No comments :
Post a Comment