Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), leo inafungua dirisha la uombaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2019/2020.
Bodi
hiyo imeboresha utoaji elimu kwa waombaji wapya pamoja na kutembelea
kambi za jeshi walizopo wanafunzi kuwapa maelekezo ya kujaza fomu kabla
ya kurejea majumbani kuomba mikopo.
Aidha,
mwaka huu, wamefanya maboresho katika muongozo wa utoaji mikopo kwa
umri wa waombaji waliopo vyuoni kwa kuongeza umri mpaka miaka 35 badala
ya 33 na wanaruhusiwa waliomaliza miaka mitano iliyopita na si miaka
mitatu.
Ofisa
Mawasiliano Mwandamizi wa bodi hiyo,Veneranda Malima amesema hayo
katika banda la bodi hiyo kwenye viwanja vya Maonesho vya Mwalimu Julius
Nyerere jijini Dar es Salaam maarufu Sabasaba.
Alisema
katika maonesho hayo wamesogeza huduma kwa jamii na wadau kwa kutoa
taarifa za wanaorejesha mikopo, wanaotaka kujua salio na wanaotaka
kulipa huku wanafunzi wanaotaka kufahamu kuhusu fedha zao za mafunzo ya
vitendo watahudumiwa.
Malima
alisema lengo la uboreshaji huo ni kutoa nafasi kwa wanufaika wengi
kupata mikopo hasa kwa waliopata matatizo kama ya kufiwa na wazazi hivyo
kuwa na uhitaji.
No comments :
Post a Comment