Monday, July 1, 2019

Amref Health Africa Tanzania yashirikiana na Azania Bank Ltd kuandaa Matembezi ya Hisani ya Kuwezesha Uwepo wa Wakunga kwa Uzazi Salama, Kupitia Kampeni ya ‘Stand up for African Mothers “SU4AM”


Shirika la Kimataifa la Amref Heath Africa limeshirikiana na Benki ya Azania (ABL) kuandaa matembezi chini ya mpango wa 'Stand up for African Mothers’, maarufu kama SU4AM, ambayo ni kampeni ya Amref Health Africa yenye lengo la kuhamasisha watu duniani kote kuhakikisha kuwa kina mama wanapata huduma ya msingi za matibabu wanayohitaji wakati wa ujauzito na vilevile wakati wa kujifungua.

Kufuatia kauli mbiu ya ‘Wezesha Uwepo wa Wakunga Zaidi kwa Uzazi Salama”, matembezi ya hisani ya SU4AM yaliyoongozwa na Mheshimiwa. Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto katika kumuakilisha Makamu wa Raisi Mama Samia Suluhu Hassan, aliongozana na Mheshimiwa. Hamad Rashid Mohamed, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii kwa Zanzibar katika viwanja vya Green Grounds, Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na maelfu ya washiriki waliojitokeza katika viwanja vya green ground, Mkurugenzi Mkaazi wa Amref Health Africa Tanzania, Dkt. Florence Temu alisema kuwa kwa mwaka huu mpango huu wa SU4AM imelenga (i) kuendelea kuhabarisha na kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa uwepo wa wakunga wenye ujuzi ili kuwezesha uzazi salama na kuepusha vifo ambavyo vingeweza kutokea hasa wakati wa kujifungua. (ii) lengo kubwa ni kukusanya fedha kwa ajili ya kuwezesha uwepo wa wakunga katika vituo vya afya ambapo matembezi haya yanalenga kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 1 za kitanzania kwa muda wa miaka mitatu ( 2019-2021) (iii) kuhamisha na kuwezesha uwepo wa wakunga zaidi kwa uzazi salama katika vituo vya afya.

Wakunga hawa ni kiungo muhimu katika kutoa huduma stahiki za afya hasa ya uzazi na wakati wa kujifungua na baada ya kujifungua, hivyo basi tunaomba na kuwasihi wananchi wote na kupitia makundi mbalimbali pamoja na mashirika na makampuni binafsi na washiriki wa maendeleo, waendelee kuchangia ili kukidhi lengo hili ili tuokoe maisha ya mama na mtoto katika maeneo yenye uhitaji Tanzania.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa ABL, Ndg. Charles Itembe , aliongea na umati uliojitokeza katika matembezi haya na kusisitizia lengo la benki hiyo katika kusaidia sekta ya afya, hasa katika afya ya uzazi kama moja ya nguzo za msingi za sera ya uwajibikaji wa kijamii wa kampuni ya ABL. "Wanawake wa Kiafrika ni nguzo ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi," alisema Itembe, akibainisha kuwa bila ya huduma za msingi za afya, wanawake katika nchi zinazoendelea kama Tanzania, wataathririka kwa vifo vya uzazi kwa kiwango cha juu ambacho kitasababisha upungufu wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Ndg. Itembe aliongeza kuwa ABL imetambua uhitaji wa kuunga mkono washikadau wengine kama Amref Health Africa katika suala la kuchangia mabadiliko chanya ya maisha katika sekta ya afya, elimu na uchumi. Katika matembezi hayo, ABL ilichangia kwa hali na mali kwa kutoa fedha pamoja na kuwadhamini wakunga-wanafunzi watakaotoa huduma ya afya ya uzazi katika maeneo mbalimbali nchini.

Tafiti zinaonyesha kuwa kina mama zaidi ya 200,000 wa Bara la Afrika hufariki kila mwaka kutokana na ukosefu wa huduma za matibabu. Aidha, asilimia 40 ya wanawake wa Afrika hawapati huduma za kliniki kabla ya kujifungua, na zaidi ya nusu yao hujIfungulia nyumbani. Vile vile, watoto milioni 1.5 wanaachwa bila mama kila mwaka kutokana na viwango vya juu vya vifo vya uzazi.

Kwa upande mwingine, utafiti wa Kidemografia na Afya wa mwaka 2015-16, ulibaini vifo vya mama vilivyosabishwa na uzazi kuwa 556 kwa kila vizazi hai 100,000– idadi hii inamaanisha kuwa takriban kina mama 30 wa kitanzania hufariki kila siku kutokana na matatizo ya ujauzito. Hata hivyo tunaamini kutokana na Juhudi kubwa zinazoendelea katika awamu hii, ya kuongeza vituo vya afya, vitendea kazi na madawa, elimu ya huduma za dharura za wakati wa kujifungua

ikiwemo na kuweka vyumba vya upasuaji katika vituo vya afya, elimu kwa jamii.. ushirikiswaji wa wadau na wafadhili mbalimbali, kiwango hicho cha vifo kitapungua kwa kiasi kikubwa.

Kwa kuunga mkono na programu ya Amref Health Africa. Itembe alisema, ABL inalenga kuchangania kwa kiwango kikubwa kupunguza idadi ya vifo visababishwavywo na uzazi Tanzania na kuhamasisha kauli mbiu ya Amref Health Africa ya; “Wezesha Uwepo wa Wakunga Zaidi kwa Uzazi Salama”.

No comments :

Post a Comment