
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ametoa tahadhari kuhusu mlipuko wa
ugonjwa wa Ebola ulioripotiwa katika nchi ya demomokrasia ya Kongo na
sasa
katika nchi jirani ya Uganda.
Waziri Ummy ameyasema hayo leo wakati
akitoa tamko kuhusu ugonjwa wa Ebola katika kituo kilichotengwa kwa
ajili ya magonjwa ya mlipuko ikiwemo wahisiwa wa Ebola endapo utaingia
nchini.
Waziri Ummy ametoa tahadhari kwa Mikoa yote
ya Tanzania, kuchukua hatua stahiki za kujikinga na kudhibiti ugonjwa
wa Ebola usiingie nchini kwa kutekeleza baadhi ya mambo ikiwemo,
kuepuka kugusa damu, mkojo, jasho, kinyesi, machozi na majimaji mengine
yanayotoka Mwilini mwa Mgonjwa mwenye dalili za ugonjwa wa, Ebola.
Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa Mkoa wa
Mwanza ni moja kati ya mikoa mitatu iko katika hatari zaidi ya kupata
Ugonjwa huo, ikifuatiwa mkoa wa Kagera,
Hata hivyo, Waziri Ummy amesema kuwa
Serikali imekwishapeleka jumla ya seti 3,500 za vifaa kinga kwa ajili ya
watumishi wa afya kupitia ofisi za kanda za MSD.
Aliendelea kusema kuwa, kutokana na tishio
la sasa tutaongeza seti 4,000 na kuzipeleka karibu zaidi na wananchi
ikiwa ni pamoja na kwenye hospitali zote za Mikoa na Wilaya kwa ajili ya
kujiandaa.
No comments :
Post a Comment