
Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa na
Uchangishaji ya Yanga Anthony Mavunde amesema wamependekeza kwa uongozi
kuanzisha wiki maalum itakayoitwa ‘Wiki ya Mwananchi’, itakakayokuwa
maalum kwaajili ya wapenzi na wanachama wa Yanga kuitumikia jamii.
Amesema wiki hiyo itakuwa ikifanyika mwezi
Agosti kila mwaka na siku ya kilele chake kutafanyika tukio kubwa
litakalofanyika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam likiambatana na
utambulisho wa wachezaji wao wapya.
“Tumepanga tuwe na Wiki ya Mwananchi’,
ambapo wanachama wa Yanga watafanya usafi maeneo katika hospitali,
masoko na kutoa misaada mbalimbali. Wiki hiyo ikikamilika tutakutana
Uwanja wa Taifa”.
Amesema wamemuomba Rais Magufuli na endapo
ataridhia tukio hilo litafanyika mwaka huu ambapo miongoni mwa mambo
yatakayofanyika ni kutambulisha wachezaji wao wapya wanane ambao
wamesajiliwa kutoka nje ya Tanzania kwaajili ya msimu ujao.
No comments :
Post a Comment